Chadema na katiba mpya

chegreyson

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2011
Posts
974
Reaction score
434
Natanguliza shukurani zangu kuchangia hoja ya katiba mpya hususani kuhusiana na chama cha siasa cha CHADEMA.
Nimeamua kwa makusudi kabisa kuanzisha hoja hii ili hisitoria ije ihukumu.Kimsingi hoja ya katiba mpya ilianzishwa na wanaharakati miaka mingi wakati wa vuguvugu la vyama vingi.CHADEMA iliichukuwa hoja hii kama mtaji wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.Chadema ilikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa wao wangeunda serikali ,KATIBA MPYA ingepatikana katika siku 100 za serikali ya CHADEMA.Hoja ya kwanza inaanzia hapo, Hivi mchakato wa siku 100 demokrasia gani ingechukuwa mkondo katika mazingira hayo.Hili watu hawataki kujadili ana kwa makusudi ama kwa kuogopa kujadili udiktenda ambao ungetokana na kuburuza Watanzania ndani ya siku 100 za kupata katiba.
Baada ya wanaharati na vyama vya siasa kuishinikiza serikali na chama tawala, Rais Kikwete alisoma alama za nyakati na kukubali mchakato wa katiba mpya,hata kama kwenye ilani yao hili halikuwa hoja.
Wakati wa mchakato wa kupeleka bungeni mswaada wa katiba mpya CHADEMA WAKARUKIA KUPITIA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE CHINI YA ANNA MAKINDA ,KUWA MSWAADA HUU UJE KWA HATI YA DHARURA.
Hati hii ilishinikizwa na Mshemiwa Zitto nailinukuliwa kwenye ansadi, pale Spika alipolieleza bunge kuwa Zitto Kabwe ndiye aliyekuwa ametoa pendekezo la hati ya dharura,kwa madai kuwa lilikuwa na uharaka ,hivyo lisingeweza kusubiri taratibu za kawaida za kibunge.
Kama kawaida hili la CHADEMA KULAZIMISHA HATI YA DHARURA halizungumzwi ana kwa makusudi ama kuficha makosa ambayo yalifanywa na CHADEMA lakini anayebebeshwa lawama amekuwa bubu.
Baada ya serikali kuleta mswaada huu kwa hati ya dharura, Chadema wakawa wa kwanza kupinga mswaada kusomwa ama kupelekwa kwa hati ya dharura ,safari kupitia kwa Mwenyekiti Mbowe.
Baada ya hapo yanayoendelea si hoja yangu kwab sasa.

Hoja yangu ya msingi ni kuwa chadema ndio waliolibiruza benge kupeleka mswaada kwa hati ya dharura, nakwa ujanja wakajinasua na CCM wao kawalala usingizi wa pono na kupokwa hoja.
Naomba kutoa hoja.
 
Magamba yalikuwa yanatoa hoja kama hizi Bungeni! Yaani badala ya kujadili hoja walikuwa wanajadili personalities, kila anayesimama lazima aitaje CHADEMA ili hoja yake kuonekana kuwa na maana! Endeleeni kumpiga chura mateke, ndio kumwongezea mwendo kwenyewe huko!
 
Nisingependa kuchangia hii thread kwani kwa vyovyote mtoa mada angeamini mie ni pro-CDM. Nachangia kwenye sehemu moja tu ya mada yako: CDM hawakutuambia watatupatia katiba 'mopya' ndani ya siku 100, walichotuhakikishia ni kuanza kwa mchakato wa kuipata. Mengine wengine watachangia.
 
Si kweli kama Chadema walisema kuwa wataandika katiba mpya katika siku 100. Alichoahidi Dr. Slaa wakati wa kampeni zake ni kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya ndani ya siku 100 za kuwa madarakani. Mwandishi unapotosha hoja kwa makusudi kama walivyofanya wabunge wa CCM & CUF na hatimaye mwenyekiti wao akaja na upotoshaji huu.
 
Umetumia muda mwingi kuandika pumbu tupu, Chadema walisema watanza mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100 kitu ambacho Kikwete pia ametekeleza ingawa kwa unafiki mkubwa
 
Hebu jaribu mradi wa kufuga kuku kuliko kukariri upuuzi wa ki-ccm, kwa mfano nani ataamini cdm walisema katiba itakamilika ndani ya siku 100. mambo haya ukiwaambia wabunge wa ccm utapigiwa makofi sana, siyo great thinkers.
 
Hongereni chadema kwa msimamo wenu thabiti juu ya kuhakikisha Tz inapata katiba mpya......... Lakini! mbona hili jambo mnataka kuliendesha kwa manufaa yenu? Kwa nn huu mchakato wa kuwaelimisha watanzania juu ya hii kitu msiwaachie wataalamu wa sheria? Na hata kama nyie mnawatu wanaojua sheria bado haiwafanyi nyie mjiingize moja kwa moja katika hili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…