CHADEMA na orodha mpya ya mafisadi


Wamekwisha fungua mashtaka kwenye mahakama ya wananchi na sisi wenye uchungu tayari tunasikiliza kesi. Tunazidi kuwaomba wenye ushahidi wazidi kujitokeza na kwa hakika tutawahukumu. Wengine wao wameanza kutumikia kifungo cha wananchi hapa hapa - kwa kuogopa hata kujitokeza kuwasalimia wanannchi. Kwa hivi sasa kesi za nyani hatuwezi kuzifikisha kwenye mahakama za ngedere.
 

Mkuu SHY nafikiri hata hii comment yako nayo ni ufisadi. Kwa nini wanyamaze wakati fisadiz wako wengi tu mpaka humu JF. Itakuwa vibaya kama na jina lako litakuwa limesahulika kwenye hiyo orodha mpya ya fisadiz. Vita hii ni kali na haiwezi kuzimwa kirahisi kama vile kuzima kibatari.
 
Kazi nzuri sana Chadema waanikeni MAFISADI wote wanaoimaliza Tanzania.
 

Kweli mkuuu,
Pia nimeona mahali fulani analo jina jingine tofauti na la Yona na kosa alilolifanya ni kuweka viashiro vyote anavyotumia hapaJF.
 
Nimeona mahali huyu Yona anajitangaza kwamba ana Masters ya IT kwenye University moja USA (nimesahau jina). Nina uhakika hii sio kweli. Huyu jamaa hana elimu kabisa kwa jinsi anavyojidhihirisha hapa.
 
Tatizo sio kutajwa...tatizo ni kuchukuliwa hatua!

At least jamii itawatambua more fisadiz kama wakitajwa. Tunakumbuka wiki iliyopita Mheshimiwa Sana JK aliahidi kuwa hatawataja FISADIZ kamwe. Kwa maana hiyo serikali haitadiriki kuwataja kwa uwazi, hivyo wapinzani watumie nafasi hii kueleimisha wananchi ni nani anahujumu hii nchi
 
Nimeona mahali huyu Yona anajitangaza kwamba ana Masters ya IT kwenye University moja USA (nimesahau jina). Nina uhakika hii sio kweli. Huyu jamaa hana elimu kabisa kwa jinsi anavyojidhihirisha hapa.

Jaribu kufukua tuone ukweli ulipo, nasi tutajaribu kutafuta ukweli.
 
Tuko pamoja Chadema kwa hili; fukueni na mpaka masangara wafukuliwe; kitaeleweka tu; wanaowakatisha tamaa wacheni watakuja kuona 2010 matokeo haya ya leo
 

Wasi wasi wangu ni kuwa wananchi sisi ni rahisi sana kurubuniwa
 
Siku zaja

Wakati watanzania watakapotaka mawazo mapya

Wakati watanzania watakapohitaji watu wapya

huo ndio wakati watanzania watakapohitaji chama kipya.

AMANI IWE KWENU!!!!!!!!
 
Wewe unamwamini? Normally the guy is shamelessly plagiarizing other people's ideas and works everywhere in his postings
 
CHADEMA wanatakiwa kutoa orodha hii mapema, ili iende pamoja na huu mchakato wa kuwaburuza KORTINI hawa mafisadi walotajwa kwenye ile orodha ya kwanza.
 
Sera zikisha unaibua sera za mabomu huwa zinalipa muulizeni mzee wa Kiraracha, Mzindakaya et al....
 
Sera zikisha unaibua sera za mabomu huwa zinalipa muulizeni mzee wa Kiraracha, Mzindakaya et al....

Tumeona matokeo ya ile orodha ya aibu, watuhumiwa ingawa si wote wamesogezwa mbele. Inawezekana ikawa ni ngonjera ya JK lakini at least wameonja karaha ya Keko. Watanzania wataendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na Fisadiz kila angle, iko siku Mungu atasikiliza kilio chetu. Kama Mungu aliweza kuwasikiliza wana wa Israeli wakiwa jangwani kwa miaka 40, Kweli Mungu atashindwa kutusikiliza sisi ambao tumekuwa jangwani kwa miaka 48!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…