CHADEMA NA WAKENYA MNAMASLAHI GANI NA VURUGU ZA NGORONGORO?
Wamasai wa Ngorongoro wamesikitishwa sana na vitendo vya CHADEMA Kuchochea vurugu Wilayani Ngorongoro Katika kata moja ya Enduleni, CHADEMA ni chama ambacho kimechochea mgogoro wa eneo letu takatifu la Ngorongoro. Tunalaani kwa nguvu zote juhudi hizi za CHADEMA kuingiza siasa kwenye maisha yetu ya kila siku, ambayo yamekuwa ya amani na utulivu kwa vizazi vingi.
Tunajua wazi kuwa CHADEMA imekuwa ikitumia mbinu za kuchochea mgawanyiko na kuchafua mazingira ya kijamii kwa lengo la kujinufaisha kisiasa. Hatutakubali kuwa ngao ya maslahi ya wanasiasa wachache wenye tamaa ya madaraka, ambao hawajali hali yetu na maslahi yetu kama Wamasai. Migogoro inayochochewa inahatarisha utamaduni wetu, mifugo yetu, na amani tuliyoijenga kwa muda mrefu katika ardhi yetu.
Tunatoa wito kwa CHADEMA na vyama vingine vya siasa kuacha mara moja kuchochea migogoro miongoni mwa jamii yetu. Tunahitaji uongozi unaojali ustawi wetu na unaoheshimu maisha yetu ya jadi, siasa safi zinazojali watu, sio siasa za migogoro na mgawanyiko tunaimani kubwa juu ya jitihada za Serikali kututafutia maeneo mbadala ya kwenda kuishi kwa Amani na Familia zetu (Msomera - Tanga). Wamasai wa Ngorongoro tutaendelea kuwa wamoja katika kulinda utamaduni wetu dhidi ya yeyote anayejipenyeza kwa nia mbaya.
Pia soma>> Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe