Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Inasemekana CCM wanajulikana sana vijijini kwani wako huko toka katika mfumo wa chama kimoja cha siasa. Kama ni kweli, je Chadema mtafanya kampeni kila kijiji? Kama hapana, sasa mtawafikiaje hawa wapiga kura? Nionavyo mimi ni vizuri kubandika picha za wagombea wenu hasa wa urais kwenye kila kijiji sehemu za public kama sokoni au gulioni ili wananchi kule wajue kuna chama kingine na mgombea urais mwingine - ile picha na neno CHADEMA (kwa wanaojua kusoma) yakiikiingia kwenye akili zao wanaweza kuiwekea tick picha ya Dr. Slaa siku ya uchaguzi watakapo kutana nayo - this is scientific. Kama hii ni ngumu, basi vetengenezwe vipicha vidogo kama A5 size ambavyo vitagawiwa kwenye mabasi yote yanayofanya safari nchini - ya mikoa, wilaya na vijiji na kumwomba kondakta baada ya kupewa token/ dispatch payment kudondosha idadi fulani ya vipepelushi hivyo kwenye stendi na wanakijiji kuokota na kupata ujumbe na picha ya Dr. Slaa ambako haijafika au haitafika kwa njia nyingine ile. Nasema hili kutokana na uzoefu wangu jinsi barua zinavyotumwa vijijini ambako hakuna posta - barua hudondoshwa kwenye stendi ya basi na wanakijiji uikota na kumpelekea mhusika, pia mara basi linapofika stendi wanakijiji ujazana ili kuokota barua, kupata taarifa za mdomo, sehemu ya kiburudisho na kadhalika.
Wazo hili ni copyrighted na ninawapa Chadema permission ya kulitumia na mwingine hasijedai right hii!!
Wazo hili ni copyrighted na ninawapa Chadema permission ya kulitumia na mwingine hasijedai right hii!!