CHADEMA ndio wamesababisha mgomo wa madaktari

Mtu wa tofauti na hapo anafuata nini humu? hii ni nyumba ya wafikiriaji wakubwa, watu wenye fikara fupi hapawafai hapa.

Ndio maana tuwe na qualifying test kabla ya kujiunga ili tuwe na cream nzuri tu !
 
dah! Uko vizur mm kama intellectual nimekusoma.
 
chadema noma....ndo walisababisha na mv-spice highlander kuzama,..pia nakumbuka hawa chadema ndo wanasababisha bei ya vitu kupanda kila kukicha, yaani chadema ndo wamesababisha na dokta mwakyembe apewe sumu afe,jamani chadema ata mafuriko ya dar intelejensia inaonyesha waliomba mungu mvua inyeshe ili ikabomoe ikulu na waliomo wafe.....nasikia nec ya cc inawatuhumu chadema kua ata mpango wa vua gamba wao ndio waliouratibu.......
 
Hii ni siri yako! Hata yale mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam na kusababisha ndugu zetu kuhamia kwenye majumba ya nguvu kule Mabwepande, ni jamaa hawahawa wakiongozwa na makamanda wao. Hawa jamaa ni nuksi!
Kweli CDM ni hatari hata wanaweza sababisha mafuriko! Upofu huo!
 
haya tuliosoma tanzania daima jana tulisoma tunajua ni aina ya kejeli,lakini kwa kweli ni kwamba tuna serikali isiyo na uwajibikaji ndiyo maana waziri akiulizwa suala anasema yeye hakuwa waziri jambo lilipotokea!
 
Majasho bora umesema ukweli kwamba Kilaza wenu Jk ameenda kupiga picha na akina Bill Gates, hivi album yake haijajaa tu, manake nakumbuka zile picha zake akibembea kule Haiti kama Kindergaten kid, 50cents, Hivi kwanini huyu jamaa anashobokea sana wazungu??

Kwa kiongozi mzalendo na aliyetimamu kamwe hawezi kuthubutu kutoa mguu nchini mwake huku nyuma akiacha mgomo wa madaktari nchi nzima unapamba moto, hata kama ndugu zake na wake zake hawatibiwi kwenye hospitali za hapa nchini.

Badala ya kutatua matatizo eti wanatoa vitisho, kuweni na huruma na wengine haimaanishi kuwa uhai wa mtawala unathamani kuliko wa watu wengine, all people were born equal, hakuna aliyezaliwa ameshika pesa mkononi, vyote tunavikuta na tutaviacha,
 
Kuhusu maslahi ya madaktari kama wafanya kazi, kwani haijulikani kwamba Serikali ya CCM imeridhia posho ya Wabunge iongezwe toka Sh 70,000 mpaka Sh.200,000 kwa siku; ambapo madaktari wenye taaluma kubwa na wanaofanya kazi ya utabibu usiku wanalipwa posho ya Sh.10,000.? Pesa zinazotumika ni hizo hizo za walipa kodi. Wao wenyewe wanadai haki yao. Hawasukumwi na CDM.

Hili ni suala la kisiasa, na uamuzi unaweza kuchukuliwa na kuboresha mishahara ya madaktari kama uongozi utaamua hivyo.

Kuhusu Mhe. Rais kukutana na Bill Gates na kumwomba atusaidie!!! Hivi sisi Watanzania hatuoni aibu kuomba omba wakati dhahabu yetu inachimbwa na hawa hawa wageni (kama Barrick) na kupelekwa kwao Merikani/Kanada, wakituachia 3% tu ya thamani ya hiyo dhahabu kama mrahaba? Tungekuwa na hisa asilimia 60 katika miradi hii ya dhahabu hatungekuwa omba omba! Hiyo ndiyo sera ya CDM.

Wakati wa awamu ya Mwalimu Nyerere, Mrahaba wa almasi/dhahabu ulikuwa 15%. Tulipokuwa tunajadiliana na wawekezaji ktk Geita Goldmines na wale wa North Mara, tulishindwa kufikia makubaliano kwa vile tulitaka tuwe na hisa asilimia 60 na wao wawe na asilimia 40.

Nakumbuka Mwalimu alitamka kwamba ni afadhali hayo madini yabaki huko huko ardhini hadi hapo tutakapokuwa na mtaji na teknolojia ya kuyachimba. Hayaozi na yamekuwa huko tangu dunia iumbwe!! Kwa sasa wachimbaji wadogo wadogo (artisanal miners) waendelee kuyachimba ambapo thamani yote (asilimia 100) inabakia humu humu Tanzania.

Wakati huo nilibahatika kushiriki ktk yale majadiliano nikiwa Waziri wa Fedha na Mipango. Kwa yale machimbo ya Buhemba, nadhani tuliweza kushirikisha JKT na kwa hiyo tatizo la wawekezaji kuwa ni wageni halikuwepo.
 
binafsi nimekuelewa hata bila kuitafakari malenge yako yako nimazuri.ila tunayafanya kinyume.
 
Nini maana ya yalitoandikwa? kwa upana zaidi ni kuwa uzembe wa serikali kutowajibika hukimbilia kutoa sababu nyepesi kwa kila jambo litokealo.

Ndo mana utasikia mwananchi akidai haki yake ya msingi ataambiwa umetumwa na CHADEMA, hivyo basi tuwaache na kauli zao nyepesi tujenge chama chetu CHADEMA ndo kuliko na uongozi wa kweli tuachane na hao watawala wa mipasho, ukiona mzazi anakaripia mtoto na hakuna utii ujue hapo pana kasoro.

2012 pana mengi yaja na wale wataalam wakuiba kura kunuka zaidi kwani haki ya mtu haipotei, walitenda wasubiri machungu yake kuyameza. Na wengine huenda wakakimbia nchi au vivuli vyao, tusali kumwomba Rab ili taifa letu liondokane na hawa wezi wa mali za wananchi na pia atujalie nguvu za kupata viongozi bora wa kututoa hapa tulipo.

Kila la kheri kwa wote wanaoliombea mema taifa letu.
 
Chadema ndiyo waliosababisha serikali ya ccm isiwachulie hatua za kisheria watuhumiwa wa ufisadi, hawa cdm wabaya sana
 
Dah, kama CDM wanaratibu mpaka mafuriko basi nadhani Ccm hakuna wanachokifanya, waondoke tu!
 
Aise hii habari imeenda na wale wavivu wa kusoma na kuelewa. Umeweza kujeza na bongo za wanajf vizuri.
 
Chadema ndiyo waliosababisha serikali ya ccm isiwachulie hatua za kisheria watuhumiwa wa ufisadi,hawa cdm wabaya sana
CHADEMA hawa ndo wamesababisha wizara ya elimu chini ya serikali ya magamba/kijani kushindwa kutatua tatizo la ufaulu mdogo nchini. Yaani CHADEMA wabaya, wanataka tu nchi isitawalike.

Kwa mloshindwa kuielewa thread:
kitendawili........
Ndani ngozi nje nyama?
 
Nimeisoma hii article tz daima nimeipenda sana.... Hawachelewi Kusema Mafuriko Yaliletwa na CDM... Ha ha ha Magamba Bana!​
 
Yaani CDM Hawa.. Wamesababisha Nyumba Yangu Kuzolewa Na Mafuriko... NDO hawa hawa CDM wamevunja ndoa yangu!
 
Licha ya kwamba makala hii na ujumbe wake vinastahili kupuuzwa na uongozi wa CHADEMA, ni vizuri tutambue kuwa wengi wa WaTz sio sophisticated kiasi cha kupuuza usemi huo. Kwa hiyo usemi huu, hasa ukirudiwa mara nyingi, WaTz wanaweza kuamini ni kweli.

Kwa hiyo jukumu la CHADEMA ni kueleza umma kwamba ni upuuzi mtupu. Madaktari wenyewe wanatambua ufinyu wa maslahi yao na hawahitaji wanasiasa kuwahimiza kujua hayakidhi mahitaji yao muhimu.
 

mh!!!!!!!! kazi kwelikweli
 
hatuchelewi kuambiwa hata kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne ni CDM wamesababisha ili kumuaibisha raisi kupitia wizara ya elimu. demokrasia bwana yaweza geuka domo la gasia wakati wowote ule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…