CHADEMA ni Kama Sikio la Kufa

CHADEMA ni Kama Sikio la Kufa

SSH Anawajibika

New Member
Joined
Nov 9, 2024
Posts
3
Reaction score
-3
CHADEMA ni Kama Sikio la Kufa

Msemo maarufu wa wahenga usemao Mfamaji haachi kutapatapa, unaakisi hali halisi
IMG_3413.jpeg
ya Chama Cha Maendeleo na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na hata uchaguzi mkuu wa 2025.

Ninashangaa kauli za viongozi wa CHADEMA kulalamikia kuenguliwa kwa wagombea wao kwenye uchaguzi, haya ni makelele ya mtu anayetaka kuzama, aliyejitupa kwenye kina cha maji marefu akijinadi kuwa anajua kuogelea kumbe hajui kupiga mbizi.

CHADEMA wanalalama tu bila hata ya kufuata utaratibu, ili kutafuta huruma kwa makosa yao wenyewe ya kutokujiandaa vema na uchaguzi.

Kama kweli wagombea wao wameenguliwa, kwa nini wanakimbilia vyombo vya habari na kuandika mitandaoni badala ya kukata rufaa kwa utaratibu uliopo?

Napata shida kujiuliza kama kweli hawa watu wapo makini au nia yao ni uvurugaji tu! Nadhani imefika wakati watu makini na watanzania kuwapuuza.

Soma Pia: CHADEMA wanatoa Tamko kuhusu hali ya Kisiasa inayoendelea nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa


Nyumba iliyofitinika haiwezi kusimama. Wenyewe migogoro ndani ya chama kila kukicha halafu unataka uaminiwe na nani?

CHADEMA, kama mmeamua kuwa chama cha siasa fanyeni siasa, kama mmeamua kuwa genge la kutafuta hela na kuleta vurugu, tutawakataa kwa sauti kubwa.

Ninawashauri ni heri mjipange upya, mkubali tu hapa mmeshapoteza, jengeni chama chenu, ili muaminiwe.
 
Kwan siku hizi mmeongezewa AFTATU kwenye ile Buku 7 mnayopewa LUMUMBA?

MNAPAMBANA SANA

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom