Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 224
- 236
CHADEMA NI MARHUMU IBN KUZIMU?
Anaandika Mo Mlimwengu.
Waliamini lila na fila vinaweza kukaa pamoja wakapingana na wahenga waliosema havitangamani. Kila kitu kipe muda sasa hivi yako wapi? Huku kwetu huwa kuna msemo mmoja kwamba ' Enjobe erafa tehurila rukuli" kwa tafsiri ambayo siyo sisisi ni kwamba swala anayekaribia kufa huwa hasikii mlio wa ala zitumikazo kwenye uwindaji. Chadema wakiwa kwenye masuala yao ya uchaguzi ya kupata viongozi hali imekuwa si hali.
Ya Ufipa yananikumbusha kisa maarufu nchini Ugiriki ambacho kilitungwa na bwana Sophocle cha Oedipus the King. Nikiwa kijiweni mzee mmoja akasema Mbowe chama kinamfia mwenyewe.
Hii ikanikumbusha na yale ya Oedipus ambaye aliambiwa atamuua baba yake na kisha atamuoa mama yake. Oedipus kusikia hivyo akahama mji wa Corinth na kwenda Thebes. Yasemwayo yapo ikatokea kweli akamuua baba yake pasipokujua na akamuoa mama yake na watoto wakapata.
Mji ukawa si shwari kutokana na hayo madhila. Oedipus kama kiongozi kwenye mji wake yakatokea majanga ya magonjwa. Ikabidi wafuatwe watabiri waweze kubainisha kipi ni kipi?
Naona tuachane na ya Oedipus maana alimtafuta mchawi nani akajikuta mchawi ni yeye mwenyewe kasababisha yote. Sophocle hana mambo mengi. Ya Kaisari tumuachie Kaisari mwenyewe. Kinachotokea upande wa CHADEMA sasa hivi ni mparanganyiko.
Taasisi yao unashindwa kuelewa nani ni kiongozi na nani siyo kiongozi. Imekuwa kama familia ya kambale hutofautishi mkubwa na mdogo wao wanajificha kwenye kichaka cha demokrasia kwa kuvuana nguo hadharani.
Mwenzako akinyolewa zako tia maji. Wako wanapimana ubavu ila sisi tunaokaa na wahenga huwa tunaelewa kwamba vita ya panzi siku zote humfaidisha kunguru, tulijua mapema fahari wawili hawakai zizi moja na ugomvi wa fahari wawili zinazoumia huwa ni nyasi.
Ukipata nafasi ya kusoma mawazo ya Robert Greene kwenye kitabu chake The 48 Laws of Power kuna vitu utaving'amua lakini hata kwa macho ya kawaida unaweza kuviona. Kwenye law ya Never outshine your master.
Hapa ndugu Tundu Lissu kapakanyaga vizuri sana. Anafurahia kelele za nje kwamba he is too intelligent kuliko boss wake. Siku zote master inabidi aonekane yuko vizuri kuliko mtu yeyote ukitaka kumfedhehesha wakati bado kashika mpini inakuwa ni hatari.
Kufanya timing nzuri ya mabadiliko. Kwenye law ya 35 Unaambiwa Master the art of timing. Je Tundu Lissu kafanya timing nzuri kupambana na Mbowe? Maana mara zote madaraka huendelea kushikiliwa na yule ambaye huweza kusimama kidete mpaka mwisho wa vita.
Ni mara chache sana madaraka kuchukuliwa na mtu anayeanza kufanya mapinduzi ya ghafla.
Hapa wataalamu wanakuambia zamu hii Mbowe kashindwa kuandaa mbuzi wa kafara (scapegoat) siku zote wanalaumu Chama Cha Mapinduzi. Mbio za sakafuni huishia ukingoni. Wameanza kushikana wao kwa wao ugoni.
Mwanadamu yeyote hutenda makosa. Wenye busara makosa hayo hujitahidi kuyamaliza ndani ya taasisi yao na wengine huamua kuyapeleka nje ya taasisi na kuyamwaga nje. Heshima na uwepo wa taasisi ni kutunza siri zake. Yakitoka nje ujue tayari maji yamezidi unga.
La mwisho ingawa siyo muhimu sana ni kuhusiana na Law ya 29 ambayo inatuambia Plan all the way to end. Wengi walioanzisha harakati ya kuwa mwenyekiti wa Chadema walishindwa kufikia hatima yao. Na wengi wao baada ya kushindwa huwa wanaondoka kwenye chama.
Siku zote hatima ya jambo ndio kila kitu. Ukiona mtu mwanzo wa harakati anadanganywa na furaha za mwanzoni tegemea mwishoni kushindwa. Ukipanga mpango na ukashindwa kutimiza mpango maana yake hukuwa mpango. Wengi tumeshindwa kufikia kwenye malengo mahsusi kwa kushindwa kuwa na subira. Mlimwengu mimi siyo mtabiri ila naziona dalili za kuelekea kuzimu.
N:B. Tundulisu katangulia kwenda stendi wakati nauli anayo Freeman. Wapiga debe wa stendi huwa wanakuchangamkia ukifika stendi. Lakini mwenye mamlaka ya kukupa siti ya kusafiria ni kondakta. Wapiga debe mara nyingi huwa ni wengi lakini kondakta huwa ni mmoja au wawili.