Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amos Ntobi, amesisitiza kuwa CHADEMA haitakubali kufanyika kwa uchaguzi wowote wa kitaifa ikiwa hakutakuwepo na maboresho na marekebisho katika mifumo ya uchaguzi.
Akizungumza na Jambo TV kuhusu kauli ya "No Reform, No Election," Ntobi amesema lengo la CHADEMA si kujitoa kwenye uchaguzi, bali kuhakikisha kuwa uchaguzi hautafanyika kabisa ikiwa hakuna mabadiliko ya kweli katika mifumo ya uchaguzi.
"Tunapozungumzia 'No Reform, No Election,' hatutumii dhana ya kutoshiriki uchaguzi, bali tunamaanisha kuwa uchaguzi hautakuwepo kabisa. Hii siyo kuhusu vyama kujitoa, bali ni kuhusu kutumia nguvu za wananchi kuhakikisha kuwa hakuna uchaguzi utakaofanyika ikiwa hakuna maboresho”, amesema Ntobi.