Nadhani upo umuhimu mkubwa sana wa kuwasilisha malalamiko kwa sababu zifuatazo.
1) Hadi Sasa NEC wanajifanya wanatenda haki, Tunataka tupate ushahidi usio na Shaka ya namna haki hiyo inavyotendeka. Je watamwita JPM kwenye Kamati ya Maadili?
2) Mgombea wa CCM amekuwa akivunja taratibu za Ukaguzi Mchana kweupe. Kwa machache tu, amekuwa akitoa ahadi zinazokatazwa na NEC Kama kujenga barabaran wkt huu wa Kampeni, kuahidi pesa n.k. Ameonesha dhahiri kuwa atabagua majimbo yatakayokuwa na wapinzani kwenye kuleta maendeleo na anafokea, anawatisha na kuwavimbia wapigakura wasiomwelewa.
3) Tumeona viongozi wengi wa Serikali wakijihisisha bila Soni na Kampeni. Tunamwona Waziri Mkuu bila Soni akifanya Kampeni Nchi mzima kwa kutumia fedha za walipa Kodi kufanya kampen kwa maslah ya Chama chake.
4) Tunaona Mawaziri bila hofu wakiendelea kutoa ahadi na kutekeleza mambo Mbalimbali kwa lengo la kuushawishi Umma.
5) Tumeona CCM ikipewa support na UDP pamoja na TLP Mchana kweupe, Ila support ya CDM kwa ACT and vice versa ikipigwa mkwara mbuzi. Tunataka tuone NEC itasema Nini kwenye hili.
6) Tumeona Dr. Mahera wa NEC Kama refa akishambulia lango na CDM. Tunataka tufaham, hulka hii refa kushambulia lango la timu moja inatafsiri Nini kadri tunapoelekea ukingoni? Je hatawabeba wagombea wa Chama chake? Mahera anaona bado anasifa ya kuaminiwa??
7) Tumeona Serikali via Police ikijiingiza kwenye kuvuruga Kampeni za CDM kwa kushambulia wafuasi wa CDM kwa matendo yaliyo halali na Kama yanayofanywa na Mgombea wa CCM. Mbaya zaidi NEC inafurahishwa na kushabikia uhuni huo. Tunataka kujua tafsiri yake ipoje.
Yapo mengi, so ni muhimu CDM na ACT wakapeleka malalamiko rasmi dhidi ya Mgombea wa CCM ili yafanyiwe kazi Mana Sasa hivi CCM na Mgombea wao ukiachia mbali kuwa wameshapanic ila ni Kama wapo juu ya sheria.