Uchaguzi 2020 CHADEMA pumzi imekata, Bernard Membe asakwa

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Kwa mjibu wa matonyaji wangu wa karibu, Rafiki yangu wa siku nyingi sana tangu kuzaliwa CHADEMA wamendelea kujipima na kuona namna gani mugombea wao wa Urais amepokelewa na jamii ya watanzania. Kuna mabishano mengi Nyuma ya kapeti kwamba Mgombea wao anachuja mapema sana hata kabla CCM hawajapanda jukwaani.

Moja ya mijadala ni kuangalia jinsi Mugombea wao wa 2020 anavyoshuka chati ukilinganisha na Lowasa aliyekuwa anapanda chati siku hadi siku.

Kwenye mazungumuzo yetu ya simu (recorded ila natunza siri ya mtonyaji wangu) Rafiki huyu amenitonya kwamba sasa CDM wako tayari kuwaachia ACT Wazalendo majimbo yoyote watakayo yataka ili mradi Membe aongeze nguvu hili jahazi linalo zama.

Tangu Mgombea wao achaguliwe hakuna mwanasiasa yeyote maalufu kutoka chama chochote aliyejitokeza na kumuunga mkono tofauti na wafuasi walewale wakati wa Lowasa CCM kilimeguka na hii iliwapa nguvu CHADEMA .

Shida nyingine ni agenda/sera gani mgombea wao atatembea nayo wakati wa kampeni. Hapa ndipo penye shida pia maana CCM wamebeba agenda zote za maendeleo. CHADEMA sasa kimebaki na agenda ya uhuru wa nyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.

Kuna shida pia iwapo CHADEMA kinataka kitembee na katiba mpya ambayo CCM wameachana nayo.. hii inawapa shida kidogo maana wakati wa bunge la katiba mpya CHADEMA walijitoa bungeni na kuwaacha CCM peke yao. Je, CCM wakitia doa hii sera itauzika?.

Inaonekana pia CHADEMA hawajafanya uchunguzi kupima nini haswa wananchi wanahitaji kwa sasa. Badala yake wamejikuta Mgombea akija na mahitaji yake binafsi ambayo hayawagusi watanzania hasa kundi la wapiga kura.

N.B. Mjumbe hauawi.
 
Hapana Lissu hajachuja kwani kampeni za Chadema zimeshafunguliwa rasmi? Subiri kipimo kitaanzia pale kwenye ufunguzi mpaka kufunga kampeni uenda anazo nondo za kutosha. Tazama.
 
Nanukuu ( shida nyingine ni agenda /sera gani mgombea wao atatembea nayo) swali kwani wakati wa kampen mgombea anakua na agenda zake au ananadi sera za chama , kwa nini mkuu unakua muongo kiasi hiki , mungu anakuona aliekupenyezea hizo tahalifa kakuingiza chaka
 
Jamaa Anataka aonewe huruma apewe nchi!
Hana sera.
Nadhani Mwenyekiti wa Chama keshaona ilo gap!
Sasa pale kijijini anatuonesha nyumbani Kwake anakosema nyumba inamabati chakavu-A mere small family yet he couldn't make it great despite ridhaa aliyopewa na wana Ikungi ndo anataka tumpe nchi???
Cant be serious.
 
Mwandishi mwenye sensitive information kutoka chama kikuu cha upinzani hawezi andika neno "mugombea" zaidi ya once.
Wewe utakuwa muuza vitunguu umeamua kupumzisha akili ambazo nazo hazina kazi ya kuzichosha.
 
Sera ni za Chama sio za mgombea. Kama hujui sera mojawapo kama hujui kwa manufaa yako na wajinga wenzako kama wewe naamini kukiita mjinga sio kosa. Chadema ikiingia ikishika dola:

1. Itapunguza % ya urejeshwaji wa pesa ya HSLB toka 15% ya sasa kwa wanufaika ambayo hata shetani hawezitoza. Pia hakutakuwa na faini ukichelewa kulipa kama hujapata ajira.

2. Fao la kujitoa litarejeshwa, mfanyakazi atakuwa huru kuchukua pesa yake mara tu atakapoachishwa kazi tofauti na sasa serikali imegeuza mifuko ya Jamii kuwa SACCOs yake.
 
Mtakutana na kichapo cha haja huko field na sio hapa mitandaoni mnakojifariji.

Watu wengi hawamtaki Lisu wanamuona msaliti.

Mimi CCM na naipenda sana tu. ILA usaliti wa Lissu ni upi?

Hata akiongea Mwenyekiti wangu, nitamwambia samahani, ili twende sawa tuambie usaliti wa Lissu ni upi tumpe haki yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…