Pre GE2025 CHADEMA, RC Mwanza na Polisi wajadili madai ya kutekwa kwa Katibu wa BAVICHA, Watatu wakamatwa

Pre GE2025 CHADEMA, RC Mwanza na Polisi wajadili madai ya kutekwa kwa Katibu wa BAVICHA, Watatu wakamatwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza imekanusha tuhuma za kuhusika katika kutoweka kwa Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) Mkoa wa Mwanza, Amani Manengelo ambaye inadaiwa alichukuliwa na watu waliojitambulisha ni maofisa wa polisi.

Manengelo anadaiwa kutoweka Februari 14, 2025, akiwa nyumbani kwa rafiki yake wa kike, Pendo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amesema watu watatu, akiwemo Pendo, wanashikiliwa kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.

Soma pia: CHADEMA Mwanza kuandamana kesho Februari 19, 2025 hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupinga mauaji na utekaji wa viongozi wao

Akizungumza na viongozi wa Chadema waliojitokeza leo Jumatano Februari 19, 2025, katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kufuatilia hatima ya Manengelo, Mkuu wa mkoa huo, Said Mtanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, amesema Jeshi la Polisi halihusiki na kutoweka kwake.

“Tumefanya uchunguzi na hakuna taarifa zinazoonyesha kuwa Manengelo anashikiliwa katika kituo chochote cha polisi hapa Mwanza. Aidha, waliomchukua kutoka kwa mtu anayefahamika kwa jina la Pendo si maofisa wa polisi,” amesema Mtanda.

====

Wako wapi hao mnaowashikiria acheni hizo sio kucheza na maisha ya watu kuna maisha hata baada ya maisha ya watu mifano ipo duniani ona yaliyomkuta Chrstopher Bageni ndio mjue Mungu yupo na anatenda

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Back
Top Bottom