Chadema shukeni ngazi za chini

Chadema shukeni ngazi za chini

erasto Samwel

Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
78
Reaction score
91
Ushauri wangu kwa Viongozi wa juu fanyeni juu chini mpeleke pesa ngazi za chini za chama za Mitaa na kata huko ndiko kuna kazi kubwa na zinahitaji pesa sana. Hizo nguvu za juu mzilete chini.

Mfano mawakala wanahitaji pesa wanahitaji chakula ili zoezi liwezekane vizuri. Kuna maeneo mawakala wa uandikishaji wa chama hawapo. Kuna watu wanajitoa kweli lakini na chama nanyi mjitoe kuisapoti msitegemee wafadhili siku hawapo.

Huku ngazi za chini ni muhimu mno hata ktk vitu tu vidogovidogo. Jimbo ukiwauliza nao wanalia kanda wanalia hakuna pesa.
 
Hatuji huko ngazi za chini, yaani unataka ruzuku tugawane na hao wa ngazi ya mtaa, watatuona kwa TV tu, hatuji.

Na kama mnasubri tuje tuwakomboe na maisha yenu magumu, jidanganyeni. Wazee wenu wamewaachia mashamba sisi tuje tuwalimie? Kwani Kenya tangu katiba mpya kuna matajiri wameongezeka? Hayo ni makaratasi tu, yanasaidia William rutto na raila kula keki
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Mzimu mkubwa unaoutafuna upinzani ni kukosa grassroots plan.Ndio maana viongozi wa juu wa Chadema wanatoa kauli za kuhujumu uandikishaji katika daftari la wapiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Hawana nia thabiti ya kuweka mawakala na kuwalipa.
Lema juzi kajiandikisha baada ya kuona kelele zake hazisaidii.
Huwezi kushinda uchaguzi bila plan ya wapiga kura wa ngazi za vitongoji,mitaa na hatimaye wilaya.
 
Back
Top Bottom