The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Sikonge, mkoani Tabora, Felix Liata, ameendelea kusisitiza msimamo wa chama hicho wa kutoshiriki uchaguzi bila kufanyika kwa mageuzi ya kisiasa na kisheria, akiwataka wanachama na viongozi kusimama pamoja katika msimamo huo.
Akizungumza Januari 31, 2025, Liata ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepoteza uhalali wa kuendelea kuongoza dola, hivyo kinachohitajika ni hatua madhubuti za kukiondoa madarakani.
“CCM tayari kilishakufa siku nyingi, hakina uhalali tena wa kuitwa chama cha siasa na kuendelea kuongoza nchi. Kilichobaki ni maamuzi magumu tu ya kukiondoa madarakani,” amesema Liata.
Aidha, amesisitiza kuwa wanachama wa CHADEMA wanapaswa kuwa na mshikamano na kuepuka migogoro ya ndani inayoweza kudhoofisha harakati za chama hicho.
“Huu si wakati wa kurushiana maneno na kuzalisha migogoro isiyo na tija. Tunapaswa kusimama pamoja kupigania haki na demokrasia kwa ari na nguvu kubwa zaidi. CHADEMA ndicho chama kilichobeba matumaini ya Watanzania,” ameongeza.
Liata pia ameonya kuwa chama hicho hakitawavumilia watu wanaotaka kuhujumu msimamo wao wa ‘No Reforms, No Election’.
“Tunahitaji ujasiri, uaminifu, na kujitoa kwa hali na mali. Hakuna atakayeachwa nyuma kwenye mapambano haya. Wote wenye nia ovu dhidi ya CHADEMA tutawashughulikia,” amesisitiza.