Pre GE2025 CHADEMA Singida walalamikia viongozi wao kukamatwa ovyo, wawataka CCM kuacha hujuma hizo

Pre GE2025 CHADEMA Singida walalamikia viongozi wao kukamatwa ovyo, wawataka CCM kuacha hujuma hizo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida kimelalamikia ĥujuma za kukamatwa ovyo kwa viongozi wanaoendesha zoezi la usajili wa wanachama kidigitali unaoendelea kwenye majimbo saba ya mkoa huu.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida,Jackson Jingu, akizungumza leo (Julai 18,2024) na waandishi wa habari amesema chama hicho kina usajili wa kufanya siasa kama vyama vingine kwa uhuru na haki hivyo hujuma wanazofanyiwa katika zoezi la usajili wanachama halina afya kisiasa.

"Tunatoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na tunapotoa taarifa hizi wawe wanasimamia misingi na utawala bora kwa kuwasihi wenzetu wa chama tawala wasifanye mambo haya ambayo yanaleta taharuki na tunamuomba RPC achukue hatua," alisema Jingu.

Kuhusu kauli iliyotolewa na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ya ushindi nje ya box la kura, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida alisema kauli yake haiwatishi na badala yake imewasaidia kujua ukweli na hivyo kujipanga katika chaguzi zijazo.

Chanzo: Nipashe
 
zoezi la gori la mkono la NAPE ni mchakato huanzia mbali sana mpaka siku ya kutangazwa Wapinzani nao waanze sasa kuweka interventions
 
Hao Ccm wanaogopa nini wakati wao ndio husesabu kura na kutangaza matokeo?
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida kimelalamikia ĥujuma za kukamatwa ovyo kwa viongozi wanaoendesha zoezi la usajili wa wanachama kidigitali unaoendelea kwenye majimbo saba ya mkoa huu.
 
CCM dhaifu sana! Yaani wanahaha hivyo nchi nzima Kwa ajili ya Chadema ambayo wao wanadai ni sawa na mtoto mchanga?
 
Kina yule mmoja alikiwa anaiba sana alizeti mashambani, Polisi hawawezi kumuacha hivihivi
 
Back
Top Bottom