Pre GE2025 CHADEMA tuhakikishieni kuwa mkipewa kura 2025 hamtarudi CCM kuunga juhudi za Rais

Pre GE2025 CHADEMA tuhakikishieni kuwa mkipewa kura 2025 hamtarudi CCM kuunga juhudi za Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Moto wa Mama Samia ni mkubwa sana, hakuna wa kuulinganisha na kiongozi mwingine aliyepita kwenye nyanja ya huduma za kijamii. Kazi hii inawavutia wengi hasa wanawake na vijana. Binafsi simuoni mtu bila kujali itikadi asiyevutiwa na kazi za Mama.

Chadema na vyama vingine vya upinzani vimekiwa vikituangusha sana kwa kusimika wagombea kwenye ngazi za urais, ubunge na udiwani ambao Wana mahaba na CCM lakini wako upinzani kibiashara TU kutuzuga.

Orodha ni ndefu lakini Slaa alirudi CCM, lowassa alirudi CCM, sumaye alirudi CCM, Lipumba, Lissu, Mbowe, Zitto wamerudi CCM baada ya kupewa nafuu na Mama kurudishiwa mali zao, kufutiwa kesi, na kurudishwa nchini. Akina Nasari, Sugu, mdee, matokeo, mkumbo, mngwila, mtolea, kitambi, john chacha na wengine wengi wote walikuwa upinzani kutuzuga lakini wakaishia ccm baada ya kupewa kura za wapinzani.

Wananchi tusiwe wajinga tena na Tena, twendeni wenyewe tukaunge juhudi za Mama badala ya kupoteza kura zetu kuwapa wapinzani ambao watakwenda kuunga juhudi za Mama kwa kupewa fedha.
 
Back
Top Bottom