CHADEMA tuheshimu Watangulizi wetu; Tusiwe kama CCM wanavyomnanga Hayati Magufuli

CHADEMA tuheshimu Watangulizi wetu; Tusiwe kama CCM wanavyomnanga Hayati Magufuli

Megalodon

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,534
Reaction score
7,866
Uchaguzi Umeisha; ni wakati wa kumpa USHIRIKIANO Lissu.

Tuweke tofauti zetu kando na tujenge chama chenye TIJA na Chenye UWEZO wa kushika Dola.

Kwa mabadiliko haya, ipo siku Chadema inakwenda kushika DOLA, I swear. You may think i am crazy……. But i am not the only one.

Kubwa zaid, Mbowe ni sehemu ya CHADEMA na kuna jitihada zake nyingi sana kwa mali na hali alizitumia kwenye chadema, hivyo na kwakuwa kampeni zimeisha, Heshima ya Mbowe ILINDWE na mchango wake utambulike na LISSU anapaswa kufahamu hili.

Huu sio tena wakati wa kuzunguka kwenye Media na kuyasemea yale ambayo hatukuwa tukikubaliana na Watangulizi wetu ; tuboreshe kimya kimya walipokosea huku tukiweka heshima mbele kwa watangulizi. HII NI ALAMA YA UMOJA.

Tusiwe kama CCM wanavyofanya kwa Mtangulizi wao magufuli. Wamefikia hatua wanaita Watangulizi wao wachawi. Hii ni dalili ya mvurugano na kukosa hekima na busara.

Hatuwezi kuwa chama Thabiti kwa kudhohofisha juhudi zilizofanywa na Watangulizi.

Hongera Tundu Lissu.

Pia soma Mikakati ya Kuitoa CCM madarakani ; muhimu Tundu Lissu awe Mwenyekiti
-
Dr Megalodon Mushy, PhD Candidate
WHO Regional Office
Rue 52, Ottawa
Canada
 
20250122_154305.jpg
 
Back
Top Bottom