CHADEMA tunawapenda ila tunawaomba sana mbadilishe kipengele hiki kwenye ilani yenu itapofika 2025

CHADEMA tunawapenda ila tunawaomba sana mbadilishe kipengele hiki kwenye ilani yenu itapofika 2025

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wanabodi,

Kabla ya kuendelea mbele ningependa kuwapongeza CHADEMA kwa kuandaa na kushiriki kwenye maandamano. Pamoja na CCM kutumia nguvu nyingi kuzuia lakini mlijitahidi sana kufikisha ujumbe wenu kwa serikali.

Leo nilikuwa napitia ilani yenu ya 2020 kwa mara nyingine na nigewaomba pale kwenye sehemu ya vipaumbele 20 muongeze kipengele cha mabadiliko ya tabia ya nchi.

Soma pia: Kuelekea 2025 Kwanini vyama vya siasa kila siku ni katiba mpya na ununuzi wa ndege? Athari za mabadiliko ya nchi kwanini hamzipi vipaumbele?

Kwa sasa nchi yetu inapitia kipindi kigumu sana kwenye suala zima la mazingira.

Mafuriko yamekuwa makubwa, ukame umeshamiri hasa kwenye kanda ya kati ya nchi yetu na hata nyuzi joto pia zimeongezeka. Hizo zote ni ishara kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanaendelea kwa kasi sana nchini kwetu.

As much as Katiba mpya ni muhimu, tume huru inahitajika na CCM inatakiwa kung'olewa madarakani lakini suala la mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi pia ni kitu cha muhimu.

Mtanisaidia kuwatag Mbowe, Mnyika na Lissu kama wana ID humu ili niweze kufikisha ujumbe wangu.

Nawasilisha,
 
Nadhani kwanza wanashugukikia suala la usalama wao kwaujumla,kwani viongozi wa kamati kuu,wamefikiwa,mzee Kibao hatunaye.
Waache kwanza wapambanie bhai.
 
Mabadiliko ya tabia ya nchi ni ajenda ya dunia awe fisadi CCM au mjamaa China lazima awe nayo katika harakati zake!
 
Hongera kwa huu uzi. Umeandika kitu cha maana sana. Mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha mgawo mkali wa umeme kwa Tanzania, Zambia na SA.
 
Back
Top Bottom