CHADEMA, tunayo ya kujifunza kwa Askofu Tutu

CHADEMA, tunayo ya kujifunza kwa Askofu Tutu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Elimu haina mwisho na hekima ni kujifunza kutoka kwa wengine:

IMG_20211226_103449_257.jpg

Kutokuwa tayari kujifunza ni kuyakumbatia mawazo mgando:

IMG_20211221_163114_082.jpg

Yetu ni madai ya uwepo wa haki, usawa, uhuru na demokrasia.

Kila mwenye hoja hizi ni mwenzetu. Hatuwezi kuwa na marafiki wa kudumu bali agenda.

Kwa kila mpambano wa kudai chochote ndani ya agenda zetu, taarifa yetu rasmi ya mshikamano ni muhimu ikawepo na ikawa wazi.

Tusimame na askofu Mwingira na hoja zake za kukemea maovu.

Aungwe Mkono Askofu Mwingira kukemea Maovu

Tusimame na Kiroboto dhidi ya watu kufungwa midomo:

IMG_20211223_225230_042.jpg

Tuungane mkono dhidi ya Kunyamazishwa

Hatupaswi kuinyamazia dhuluma.
----------

Ninakazia:

Polepole pole ila Omba japo Msamaha Ulitukwaza wengi
 
POle michita slow naona tisiiiaraei wamesepa na ufunguo🏃.
 
POle michita slow naona tisiiiaraei wamesepa na ufunguo🏃.

Ninapata ukakasi wapigania haki tunapoingia mitini na kuwaacha wenzetu kula na wa kwao.

Yanayompata Mh. Mbowe ni mwendelezo wa kutochukua hatua zozote za mshikamano hata za kutoa matamko tu.
 
Ninapata ukakasi wapigania haki tunapoingia mitini na kuwaacha wenzetu kula na wa kwao.

Yanayompata Mh. Mbowe ni mwendelezo wa kutochukua hatua zozote za mshikamano hata za kutoa matamko tu.
Tunahitaji kuwafunza jambo wale wanaotuhujumu huku wakijidai kupambana pamoja nasi, yanayo mkuta Polepole SII ya kufurahia ila wengine wanaweza kujifunza kupitia matukio kama haya. Ila ni wenye uwezo wa kupambanua mambo Kwa upande Fulani . Hivyo ikiwa wenye nafasi na uelewa wakiacha usaliti Kwa mambo yenye manufaa Kwa taifa Kwa pamoja tutafanikiwa kuifikia Tanzania iliyo Bora
 
Ni muhimu kutenganisha hoja na watu na utu au ubinadamu wao.

Kuunga mkono hoja zenye mashiko, rasmi na wazi wazi zitatufikisha kwenye Tanzania iliyo bora mapema zaidi.

Yako wapi matamko rasmi ya vyama kumwunga mkono Askofu Mwingira?

Pamoja na ukakasi wa Polepole kama mtu, hoja yake dhidi ya kunyamazishana ni muafaka.

Yako wapi matamko yetu rasmi ya kukazia kwenye harakati za kumnyamazisha?

Mwendelezo wa kukosekana matamko rasmi kama hayo tunayaona kwenye kesi ya Mbowe.

Ni lazima kutoka katika vicious circle hii.

"Kunyamazia uovu wowote ni kujipanga na watesi wetu." Maneno kuntu kabisa kutoka kwake Desmond Tutu.

Ukweli mchungu, tunapaswa kubadilika.
 
No freedom of speech in the country. Freedom of speech pekee iliyopo ni kuwasifia watawala

Freedom of speech hawawezi kutupa bila ya kuipigania. Wamezowea kuabudiwa wanadhani ni haki yao.

Kuipigania si rahisi tusipokuwa tayari kuikemea dhuluma bila kujali inamhusu nani ni heri tukasau.

Agenda ni za kudumu, si watu.
 
Kutetea haki ya mtu wakati mwingine kunataka ujasiri, nimejifunza hili pale ambapo anayenyimwa haki yake akawa na historia mbaya kabla kwa maneno yake au matendo, wengi watishia kumlaumu kwa yale aliyofanya yaliyowaudhi lakini ni wachache sana watakaokumbuka kumbe hata kama ana makosa aliwatendea lakini bado ana haki yake.
 
Yesu alirejesha sikio la askari Jahudi lililokatwa na mtume Petro katika kumhami Yesu asikamatwe.

Tutu alimwokoa police informer wa makaburu aliyeingia kwenye 18 za waliodhamiria kumtoa roho.

Kwa kutomwunga mkono rasmi hadharani, wazi wazi na kutokuchelewa Mwingira ni ukakasi mkubwa kwa awaye yote.

Kwa kutokukemea wazi wazi, hadharani na bila kuchelewa kunyamazishwa kwa Polepole kwa awaye yote hakumkomoi Polepole, hakutasaidii bali kunampa mtesi wetu nafasi ya kuendele za dhuluma zaidi zikwamo dhidi yetu.

Tunatokaje kwenye rojo hili?

Huu ndiyo.ulio ukweli mchungu.
 
Back
Top Bottom