Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
Habari za sasa hivi wanaJF, kama ilivyo kawaida kuwaletea habari mbalimbali ambazo zinafika kwenye meza yangu kuhusu chama chetu CHADEMA huwa siachi kuwaeleza ili kupata ufumbuzi.
Morogoro ni moja ya mkoa muhimu sana kimageuzi hapa nchini, lakini nieleze wazi kuwa mwaka huu kuna tatizo limetokea, ni either sisi au kuna mchezo umefanyika kutoka upande wa pili.
Hapa tunavyoongea kuna majimbo manne ambayo tayari wagombea wa CCM wamepita bila kupingwa, hili halipo sawa kabisa.
Huu mkoa inahitajika nguvu kubwa sana kuuweka sawa ili tuweze kuvuna kura nyingi za madiwani, wabunge na Urais.
Hapo jana mgombea wetu Mwenza Salum Mwalimu alikuwa Morogoro na kilichotokea ni aibu kubwa sana, hii pengine inatokana na kutoweka nguvu za kutosha kwenye mkoa huu.
Mkutano wa kampeni wa Salum mwalimu ulikuwa mtupu kabisa kitu ambacho kimenifanya nishtuke na kuona kuna namna kama wanamabadiliko na wapenda upinzani nchini tuweke nguvu za kutosha huko.
Niliwahi kuambiwa kuwa kuna kitu alikifanya Devotha Minja, cha kutowalipa baadhi ya wale bodaboda wanaonogesha msafara na kampeni. Hivyo ni kama wamesusa( ikumbukwe wapo baadhi wanaojitolea lakini wengi huwa wanalipwa, hii ni kwa vyama vyote asije kukuongopea mtu).
Hivyo siku ya jana mkutano ulikuwa mtupu sana, ninawaomba wanachama wenzangu na wapenda mabadiliko wote tuwekeze nguvu nyingi mkoa huu.
Chini ni picha na video za mkutano wa mwalimu huko Morogoro
Sasa hivi nitakuwa naweka na video ili kuondoa maswali ya hapo ni asubuhi, mara sijui nini na blah blah nyingi