LGE2024 CHADEMA: Uandikishaji wa Majina Uchaguzi Serikali za Mitaa una kasoro nyingi

LGE2024 CHADEMA: Uandikishaji wa Majina Uchaguzi Serikali za Mitaa una kasoro nyingi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
CHADEMA kimesema kuwa hakiridhishwi na mchakato unaondelea wa uandikishaji wa wapiga kura kwani kuna kasoro ambazi zimejitokeza.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amebainisha changamoto hizo ambazo ni

1. Uandikishaji wa watoto ambao hawajafikisha miaka 18
2. Waandikishaji kuruka namba kwenye daftari la uandikishaji
3. Uwepo wa vituo nyumbani kwa viongozi na majengo ya CCM

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema akizungumza leo Oktoba 15, 2024 mbele ya waandishi wa habari juu ya zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye daftari la wakazi katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho amesema kuwa zoezi hili lina kasoro nyingi za kisheria

Mambo ambayo haturidhishwi nayo mpaka sasa, na ambayo ni kinyume kabisa na kanuni na sheria za nchi yetu. Jambo la kwanza, vituo vya uandikishaji kuwekwa nyumbani kwa viongozi wa CCM au kwenye majengo ya CCM. Kule Mbokomu kijiji cha Korini Kusini, kitongoji cha Rau KDC jimbo la Moshi Vijijini, kituo cha uandikishaji kiliwekwa nyumbani kwa mwenyekiti wa CCM, tuna ushahidi. Pili, jimbo la Rungwe kata ya Ikonjola kituo cha uandikishaji kimewekwa kwenye jengo la CCM na jana viongozi wetu tuliwaagiza waende, na tumemtaka msimamizi hicho kituo kiondolewe kwenye jengo hilo la CCM."

"Jambo la pili, waandikishaji kuruka namba kwenye madaftari ya uandikishaji, yaani wanaruka misitari hawaandiki namba na tunaamuni lengo lao ni kuja kuingiza majina feki baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika, na haya mambo yamefanyika maeneo mengi sana ya nchi yetu."

Kuandikishwa kwa wanafunzi ambao hawajafikisha umri wa miaka 18 na kuendelea, jambo hili tumeliona kule Chato mkoani Geita, wanafunzi wa shule ya bweni ya Jikombe waliandikishwa kwenye daftari. Pili, tumeona kule Mlimba wilaya Kilombero mkoani Morogoro, wanafunzi wa shule ya sekondari Mbugu, Londo na Kilamsa wameandikishwa kwenye daftari. Hapa Dar es Salaam tumeona kule Ukonga kata Kitunda mtaa wa Kiyombo, kituo cha Kiyombo shule ya msingi wanafunzi wamepelekwa na walimu wao kwa ajili ya kuandikishwa, hawajui hata umri wao. Kule Mwanza Nyamagana kata ya Nyegezi, mtaa wa Mchenga kituo cha sekondari Nyabulogoya, wanafunzi waliletwa na waliandikishwa zaidi ya wanafunzi 102 kituo hicho."

"Kituo ambacho tumegundua ni kwamba wanafunzi hawa, wote wakiulizwa umri, wamefundishwa wanataja wamezaliwa mwaka 2005 na wengine mwaka 2006, hakuna anayetaja umri tofauti na hapo. Kwa sababu kwenye vituo tuna mawakala, kwa hiyo wanafunzi hawa wanapoulizwa wataje umri, kila mmoja anasema amezaliwa 2005 au 2006 hamna anayeenda mbele ama kurudi nyuma ya hapo...Tuna watahadharisha wazazi watoto hawatopiga kura siku ya tarehe 27, Novemba 2024, na wasikubali huu mchezo. Kama chama tutajiandaa kuwazuia watoto kupiga kura ni kinyume cha sheria. Kwa hiyo wazazi wachukue tahadhari kuwalinda watoto wao wasitumike kisiasa." - Mrema.
 
CHADEMA kimesema kuwa hakiridhishwi na mchakato unaondelea wa uandikishaji wa wapiga kura kwani kuna kasoro ambazi zimejitokeza.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amebainisha changamoto hizo ambazo ni

1. Uandikishaji wa watoto ambao hawajafikisha miaka 18
2. Waandikishaji kuruka namba kwenye daftari la uandikishaji
3. Uwepo wa vituo nyumbani kwa viongozi na majengo ya CCM
1:Lema alishatoa mapovu
2: Mrema katoa mapovu leo
3: Tunamsubiria Mzee Mbowe nae
Hapa Msigwa aliposema hii ni SACCOS ndio mjue aliimanisha nini
 
Sasa kosa liko wapi kusema walizaliwa 2005/6? Hilo linawezekana kabisa kwa kizazi hiki tulichonacho hawapishani sana umri tofauti na sisi tuliosoma enzi za Nyerere na Mwinyi
 
Sasa kosa liko wapi kusema walizaliwa 2005/6? Hilo linawezekana kabisa kwa kizazi hiki tulichonacho hawapishani sana umri tofauti na sisi tuliosoma enzi za Nyerere na Mwinyi
Hapo nami nimewaza maana kweli Kuna Kuna wanafunzi wengi wamezaliwa miaka hiyo hapo labda Sasa wangeomba uthibitisho wa cheti ili kujiridhisha kama kweli Wana miaka tajwa ila kuwazuia sio sawa
 
Back
Top Bottom