Uchaguzi 2020 CHADEMA ukiingia mitandao ya kijamii huoni hotuba za mgombea kwa urefu badala yake, pilikapilika za mapokezi

Uchaguzi 2020 CHADEMA ukiingia mitandao ya kijamii huoni hotuba za mgombea kwa urefu badala yake, pilikapilika za mapokezi

El Roi

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2020
Posts
297
Reaction score
537
Kuna wakati hapo nyuma, ambao baadhi yetu tulitilia Shaka Sana organization ya Chadema ktk Mambo kadhaa wakati huu wa kampeni. Kuna Mambo mengi wamefanyia marekebisho nakubali na Mambo yako sawa.

Suala ambao bado naona hawatutendei haki sisi ambao tunakuwa hatupo physically kwenye mikutano ,ni vile wanavyosambaza taarifa na kutaka kutufanya kujua kinachoendelea kwa kutumia vyombo vya habari na niwe wazi social media.

Campaign na hasa hotuba za wagombea wengine, mfano JPM tunazipata vema na tunaelewa anacholenga even in our absence. Na hii ni kwa sababu tunafuatilia tvs ambazo zimempa enough air time campaign zake.

Nimefuatilia ACT nao wanafanya vizuri. Ukiingia you tube kwenye mikutano anayofanya zitto utapata kila uhondo na hasa hotuba zake kwa urefu na unaelewa contents na context ya hotuba zake.

Chadema wao, inashangaza! Ukiingia you tube,face book hasa, huoni hotuba za mgombea kwa urefu, badala yake ni kuonyeshwa tu, pilikapilika za mapokezi ya mgombea na mafuriko.

Suala linalosumbua Sasa ni what matters most? Ni kuona mafuriko, pilika za watu au ni madini kutoka kwa mgombea? Nijuavyo mie what matters most ni hotuba za mgombea.

Huyu ndo anaweza swing kura manake watu watapata ujumbe. Kinachotakiwa ni kura, na bila kuwa na means zitakazofanya ujumbe wa mgombea uwafikie watu ili waamue, Kuna hatari ya kutofikia baadhi ya wapiga kura hasa watu wanaotaka kujua sera na malengo ya mgombea.

Ujumbe ndo tunaotaka kusikia. Rusheni message za mgombea zote. Tafuteni namna apate awafikie watu clearly. Clips mnazorusha tena muda kidogo za mafuriko na mengine haisaidii kutuvuta baadhi yetu wapiga kura maana what moves some of us are messages and not otherwise.

Mnapoanza round nyingine hakikisheni mnafanyia kazi ushauri huu. Naona hatari mbele ya mgombea wenu, ambaye frankly speaking ni mzuri,, kukosa kura kadhaa ambazo Kama social media ingetumiwa vizuri kurusha hotuba zake fully, ingewaongezea kura.wapi watu wa idara ya habari ya chama mnapokwama?
 
Sawa tutalifanyia kazi ila hizo clip ukiziunganisha si unapata main them?

Hiyo pia ni njia ya kumkwepa msajili wa vyama na Tume ya ccm
 
Nashangaa CDM kutokusambaza sera za mgombea na agenda zake, in short CDM inahitaji akili mpya na kujipanga hivi hata kurusha facebook tu hawawezi au websites na youtube
 
Non part

Non partisan just a patriotic voter and stateman. ( Sina chama, ni mpiga kura na mzalendo asiyetiliwa Shaka)
Juzi tu umeiponda CCM kwa nguvu ya kiwango cha mamba. Leo unapulizia. Ni umalaya au ujuha? Ni kama unajitekenya na kucheka wewe mwenyewe.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Hawataki hotuba lengo kuitoa ccm na magufuli wake
 
Back
Top Bottom