Mkuu Pasco, conventional wisdom inakubaliana nawewe kwa kila kitu ulichoandika hapo juu. Hata mimi nakubaliana nawe. Ingekuwa rahisi kukaa kimya na kutosema chochote, kwangu mimi ingekuwa unafiki. Debate kali sana ilifanyika live hapa jamvini kati yangu na Zitto (au wale wanaomuunga Zitto) hivi karibuni.
Kumbuka kuwa hizi debates hazikuanza leo, zimekuwepo toka kipindi cha buzwagi na zitaendelea kuwepo. Hata leo hii chama cha Obama US bado kuna internal debates za kati ya liberal na conservative democrats.
Haya ni mambo ya kawaida sana kwenye vyama vikubwa. Chadema ni chama kikubwa na tofauti za kisera na mwelekeo zipo na zitaendelea kuwepo. Vyama ni mkusanyiko wa watu na watu wanafikiria tofauti.
Kuacha hayo yaliyopita, inawezekana matumizi ya neno kufuatilia yamekukwaza. Nilitafsiri tu toka kwa sentensi ya kingereza (I have been following). Bahati mbaya, wengine wetu ambao bado tuko shuleni, inabidi tufikirie kwa kingereza all the time ili kufanya home works. Hilo neno kufuatilia halikuwa na maana nyingine mkuu Pasco.
All is well, we enjoy picha ....asante