Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Waswahili wanasema ukiwa Muongo jitahidi kuwa na kumbukumbu, Jana mkurugenzi wa halmashaurimya wilaya ya KILOSA Ndugu MICHAEL GWIMILE alisema hawajawaengua kabisa wagombea wa CHADEMA na kwamba kila kitu kinakwenda sawa na kufuata kanuni, sheria na taratibu za kiuchaguzi, sasa hizi ni namba za VIJIJI 24, VITONGOJI 118 na wajumbe wa Halmashauri za vijiji 242 ambao wameenguliwa bila kufuata kanuni za uchaguzi na leo walipopeleka mapingamizi ( kukata rufaa ) wasimamizi wasaidizi wamefunga ofisi zao na wengine wamekataa kupokea barua zao za rufaa, Tumemuandikia barua Msimamizi mkuu wa uchaguzi yaani mkuruĝenzi kumwambia huo ubatili na hujuma zinazofanywa na wasaidizi wake , TUNASUBIRI MAJIBU na wagombea wetu wote kurejeshwa mara moja na kupata HAKI yao ya kikatiba.
Soma pia: Morogoro: Msimamizi wa Uchaguzi Kilosa amjibu Joseph Haule (Prof. Jay) kuhusu Wagombea wa CHADEMA kuenguliwa