CHADEMA wahitimisha mabaraza ya rasimu NCHI NZIMA

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575

[TD="bgcolor: #ffffff"]


[TD="bgcolor: #ffffff"]




KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, leo anahitimisha siku 15 za ziara ya chama hicho ya kukusanya maoni ya rasimu ya Katiba mpya iliyofanyika nchi nzima, ukiachilia mbali mikoa ya Lindi na Mtwara ambako Jeshi la Polisi lilizuia mikutano hiyo.

Taarifa ya ofisa habari wa chama hicho, Tumaini Makene, ilisema kuwa timu ya katibu mkuu leo itahitimisha mabaraza hayo ya wazi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
Tangu Agosti 12, mwaka huu, CHADEMA kupitia timu zake mbili za viongozi, wakiongozwa na mwenyekiti na katibu ilianza ziara ya kukusanya maoni ya rasimu ya Katiba mpya kupitia mabaraza ya wazi.
Timu ya kwanza iliyoongozwa na Mbowe ilipita katika mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Tabora, Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe na kuhitimisha Iringa juzi.
Dk. Slaa na timu yake wao walichanja mbunga katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Singida, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam na kisha timu hizo mbili zitaungana kuelekea visiwani Zanzibar.
Katika mikutano yao, wananchi mbalimbali waliweza kutoa maoni yao kwa kuzungumza na kujaza fomu maalumu juu ya mambo wanayotaka yazingatiwe kwenye Katiba mpya.



[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
[/TD]
[/TD]
 
Duh!! Hao jamaa wako vizuri na kimtindo chao cha kutumia Chopa.
Wanastahili kupongezwa maana wanakuja huku huku mitaani na vijijini kwetu kuchukua maoni yetu.
Kuna haja kwa CCM kuiga huu mtindo wa CHADEMA maana unalipa sana kisiasa.
 
CHADEMA wanatwanga maji kwenye kinu. Kwanza Warioba alishawaambia hatapokea maoni yao. Pili, CCM imechukua fomu zao na kuzijaza HAPANA hasa sehemu ya serikali tatu. Tatu, CCM inayashinikiza mabaraza ya wilaya kutoa mawazo ya chama na wamefanikiwa sana kwa hili hasa kukataa serikali 3.
Kwahiyo nyie CHADEMA hamna kitu kwa suala la katiba labda kipindi cha kura ya wananchi mkikazana hapo kutoa elimu hasa vijijini ambako mnaogopa kwenda mtafanikiwa; vinginevyo mpende msipende Katiba ya CCM itapita tu. Pitia pia post hizi:
https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/508133-butiku-ningejua-ccm-itaingilia-mchakato-wa-katiba-nisingeshiriki-new-post.html

https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/500954-warioba-hatutachukua-mawazo-ya-katiba-majukwaani-wala-kwa-mashinikizo-ya-vyama-vya-siasa-new-post.html
 

Hebu rejea LINK ya pili uliyoiweka na uilinganishe na ile ya kwanza na post yako!
Huoni unajichanganya?
Itakuwaje Warioba akatae mashinikizo ya vyama vya siasa halafu ayakubali mawazo ya CCM?
Au CCM si chama cha siasa?
Na kama hatapokea mashinikizo ya vyama vya siasa, itawezekanaje akubali kutengua uamuzi wa TUME wa kupendekeza serikali tatu?!
Kumbuka pia kwamba Warioba alishasema kwamba mawazo ya Mabaraza yatachaambuliwa na kuangalia lipi ni wazo binafsi na lipi la kutumwa-hasa CCM!
Kwa upande mwingine, elimu ya umuhimu wa serikali tatu iliyoenezwa na CHADEMA imetosha kuwaamsha watanganyika na hivyo, kama rasimu itakayopitishwa ni ile ya CCM; kura ya maoni itaamua....
Mnapoandika kumbuka jukwaa lina watu wenye vichwa vilivyopikika vyema!
Serikali tatu haziepukiki ndugu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…