CHADEMA wakishiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wasije kwetu kulalamika wameibiwa kura....wameyataka wenyewe

CHADEMA wakishiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wasije kwetu kulalamika wameibiwa kura....wameyataka wenyewe

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Salama ya CHADEMA nikususia uchaguzi zaidi ya kushiriki. Wawaache wale ambao wana tamaa ya ubunge waende ACT au CHAUMa kuliko kushiriki uchaguzi unaosimamiwa na Makada wa CCM.

Wasipoweka msimamo wanakwenda kuchakachuliwa vyakutosha na kisha kupelekwa kwenye meza ya maridhiano
 
Watie nguvu katika upatikanaji wa tume huru, lasivyo watakandwa vibaya.
 
Salama ya CHadema nikususia uchaguzi zaidi ya kushiriki. Wawaache wale ambao wana tamaa ya ubunge waende ACT au CHAUMa kuliko kushiriki uchaguzi unaosimamiwa na Makada wa CCM. Wasipoweka msimamo wanakwenda kuchakachuliwa vyakutosha na kisha kupelekwa kwenye meza ya maridhiano
Maaamuzi ya taasisi yatafanyika kulingana nyakati, ccm kama mnajizungusha ili ikifika mda chadema wasusie uchaguzi ili mje na mapandikizi yenu kutoka kwenye vyama vya mfukoni , jipangeni tena,

Ccm itavulumishwa madarakani tu bila kujali mizengwe yoyote mnayotengeneza, chadema wapo mbele ya wakati
 
we chawa tuje kwenu kama nani wewe? Chadema mbona inawawasha sana?
 
Wasusie na njaa Kali waliyo nayo Sasa hivi.Thubutu.Watajitahidi wapate ubunge na ruzuku.
Hawana ubavu wa kususia
 
Hakuna mtu atasusia,

CDM haitosusia,

Wananchi pia hatutosusia,

Tutahakikisha Sanduku la kura linarudi mahala pake Ili tuchague viongozi wetu Kwa HAKI.

Tofauti na hapo, uchaguzi wa HAKI hautofanyika.
 
Salama ya CHADEMA nikususia uchaguzi zaidi ya kushiriki. Wawaache wale ambao wana tamaa ya ubunge waende ACT au CHAUMa kuliko kushiriki uchaguzi unaosimamiwa na Makada wa CCM.

Wasipoweka msimamo wanakwenda kuchakachuliwa vyakutosha na kisha kupelekwa kwenye meza ya maridhiano
Kwa nini usiseme tu wazi hapa kuwa unawafanyia CCM kampeni ya kuendelea kutawala milele; kuliko kusumbua akili za watu na mada ya ajabu sana kama hii?

Unataka CHADEMA wasusie, ... halafu iweje? Ili CCM waendelee kutawala bila ya usumbufu wowote!

Naona unahangaika sana hapa kuweka mada nyingi JF, hiki kihelehele ni cha nini hasa?
 
Back
Top Bottom