CHADEMA wakisusia maridhiano watasusia na vikao vya kuandika Katiba Mpya?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Nilimsikia Rais Samia akisema ataunda tume ya maridhiano nchini ya kuwaleta watanzania pamoja kabla ya kuanza mchakato wa kuandika Katiba mpya. Nimewasikia chadema wakisema hawatahusika wala kushiriki kwenye maridhiano. Kwa maoni yangu sioni namna chadema itakavyoshirikishwa kwenye kuandika katiba mpya kama itagomea maridhiano.

Baada ya mgogoro wa wakati na baada ya uchaguzi ni maridhiano pekee yatakayoweza kuwarudisha chadema na CCM kukaa kwenye chumba kimoja na dawati na kujadili kitu kimoja. Nahisi dalili za chadema ama kuchelewesha, kutengwa au kuzuia uandishi wa Katiba mpya. Watakuwa kama UKAWA mwingine waliozuia mchakato wa umalizaji wa uandishi wa katiba mpya. Na hii itakuwa ni faida kwa CCM zaidi (status quo).
 
Hakuna Maridhiano wala Katiba mpya bila CHADEMA kushirikishwa kikamilifu.
 
Hakuna Maridhiano wala Katiba mpya bila CHADEMA kushirikishwa kikamilifu.
Akili mbovu kama hiyo itawatia hasara kubwa sana. CCM inaweza kuongoza nchi hata kama chadema wamenuna kama vifutu. Nendeni na slogan ya win-win angalau muambulie kitu kidogo.

CCM wana kila kitu cha kuwafanya waweze kuongoza bila ya kujali chadema wana hali gani. CCM kuna wakati ilivifungia vyama vyote hakuna kufanya siasa na ikawa hivyo. CCM ilishawahi kuwaengua wagombea wote wa upinzani na ikawa hivyo. TAL aliwahi kutandikwa vibaya sana kwa risasi na mambo ya nchi yakaenda tu. Viongozi wa upinzani walishawekwa ndani kwa muda mrefu lakini taifa likaendelea na mambo yake. CUF kule ZnZ ilishawahu kupokonywa ushindi mara kadhaa lakini mambo ya nchi yanakwenda tu.

Mwalimu aliwaasa na kuwaonya wapinzani kuwa waende wengi bungeni yanakojadiliwa mambo ya wananchi lakini sio kuitaka Ikulu harakaharaka kama hivi bila kuwa na sera na watu wa kutosha.

Hakuna mlevi hata kwa bahati mbaya atampa Lissu nchi aiongoze, over my dead body!!! na kama mnabisha, just wait and see. Hata mm mtu wa kawaida maisha yangu yataboreka kama bunge litakuwa na nguvu ya vyama vingi kuliko chama kimoja. Shirikini maaridhiano ili muambulie vipapatio vya ajira na ruzuku.
 
Bila chadema huwezi kufanya maridhiano wala kuandika katiba, maana chadema ni sauti ya wananchi walio wengi
Amekudanganya nini kuwa chadema ni sauti ya waliowengi? Hama vurugu zile za uchaguzi ilibidi watu wajitokeze kwa kulipwa, kuahidiwa na kuleta watu kutoka nje. Watu wengi bro huwezi kuzizima sauti zao kwa kitu chochote kile. Watu wengi hawajawahi kufeli kwenye jambo lao. Zile vurugu zilizimwa kama kibatali kwasababu hakukuwa na hiyo nguvu ya umma unayodai ipo. Ipo wapi kaka wakati Lissu yuko kampasi ya lupango?. Chadema ilisusa uchaguzi lakini mbona maji yanaendelea kutoka kwenye mabomba hata ya viongozi wa chadema? Mbona umeme unawaka kote Mbona magari yanaendelea kutembea kwenye barabara zilezile za kabla ya uchaguzi? Tuache kujidanganya hatuna cha kufanya zaidi ya kuungana nao kwenye hayo maridhiano kwa manufaa ya taifa na chadema pia.

Hii nchi ni kubwa kuliko sisi wote mmojammoja au hata watanowatano au hata vyama vyetu. Kuna watu lazima uhuru wao ulindwe na serikali kwa nguvu zote kwakuwa katiba yao inasema hivyo.
 
We unahisi kutakuwa na lolote katika hiyo katiba mpya inayozungumzwa sasa.? Hata ingekuwa mimi chadema ningesusia. Ujinga mtupu.

Kwann tusiendelee alipoishia tume ya Warioba? Kwamba mnataka muanze mchakato mpya.

Mzee Chande anaongea vitu mtu unawaza hata hupati jibu yaani. Anasema eti wakati w mchakato wa mzee Warioba kuna watanzania walikuwa na umri mdogo na sasa wangependa kushiriki dah. Kwahiyo kwa tume hii anayoshauri yeye baada ya miaka 10 inabidi mambo yabadilishwe maana hawa madogo wa sasa hivi si watakuwa watu wazima that time na hawakushiiki?
 
Unakatwa
 
Na Katiba mnayoishadadia itakuwa ni ya wananchi kweli au tutapigwa tena changa la macho kama ile Katiba pendekezwa ya Kikwete?
 
Kwanza, Nchi nzima inapata hasara kwa utawala mbovu wa CCM, hata nyie machawa mnataseka na utawala wa CCM, sio viongozi na wanachama wa CHADEMA tu. Wanaofaidi nchi hii ni kakikundi kadogo tu ndani ya CCM na wanamtandao kwa hiyo msijidanaganye na kujifariji na utawala wa CCM mkikenua meno mnapoona Lissu na wenzake wakidhulumiwa.

Pili, CHADEMA na wote wenye akili wameshazichoka siasa za CCM za danganya toto za kuambulia makombo kidogo tu. Hii nchi raia wameshazinduka kwamba inaliwa na kakikundi kadogo tu ndani ya CCM sasa na wao wanataka kushiriki kikamilifu kufaidi kodi na rasilimali zao kama raia kamili, nakuhakikishia CCM haitaweza kuwarudisha kwenye chungu tena.

Mwisho, Hakuna mtu anataka Lissu apewe nchi, Kwa sababu imesemwa hii ni nchi kidemokrasia watu wanataka uchaguzi wa haki na kweli chini ya tume huru na katiba mpya. Halafu kama mama yenu ameweza kuwa rais hata Yericko anaweza kuwa rais achilia mbali Lissu.
 
Wasomi wa sasa kwa asilimia kubwa ni watumwa wa wanasiasa.
 
Hata wakishiriki hakuna maana yoyote sababu katiba itakayoandikwa chini ya utawala wa CCM ni kama report ya Chande tu.

Akili zipo kwenye kubaki madarakani na kuzuia uwezekano wa wengine kuchukua mamlaka waliyojimilikisha.

Badala ya kuandika KATIBA MPYA jina tu,heri isiandikwe kabisa.
 
Huu mchakato wa kuandika Katiba Mpya unavyokabidhiwa kwa CCM na serikali yake, ndio kosa la kwanza linapoanzia hata kama hiyo katiba kweli itaandikwa itakua na kasoro.

Sioni kwanini CCM wapewe nafasi kubwa ya kusimamia huo mchakato ikiwa Katiba ni hitaji la watanzania wote.

CCM haiwezi kuandika katiba mpya ikiwa hii mbovu iliyopo inawanufaisha wao, sasa kwanini waandike mpya?

Ni kama vile wewe mwandishi wa hii mada ubadilishe suruali yako au shati ambayo haina tatizo, tena ile ambayo ukivaa unasifiwa umependeza.

Naona itatuchukua muda mrefu sana kupata katiba mpya ya kweli tuitakayo, kama bado tunakosea hatua ya mwanzo kila tukitaka kuanza mchakato wa kuitafuta.
 
Kama vile walivyoibadilisha jina NEC ikawa INEC wakasema tayari ni tume mpya huru ya uchaguzi.
 
Hatutaki katiba ya kuandikwa na wanasiasa. Iliyopo imeandikwa na ccm ndo tunayopinga. watu wanataka katiba itakayo andikwa na wananchi. Chadema wanapigania katiba mpya hawapiganii kuandika wao katiba. Halafu nyie ccm kila kitu mnawaza wanasiasa tu, hivi hakuna watanzania kwenu wenye akili zaidi ya wanasiasa. Katiba zote bora duniani hazikuandikwa na vyama vya siasa. Huwezi ukawa chama cha siasa halafu ukaandika katiba yenye maslahi kwa taifa.
CCM wameandika katiba, wamerekebisha na kuihuisha mara kadhaa lakini bado haifai kwa sababu mambo yote yaliyomo yanareflect maslahi ya ccm tu na sio maslahi ya Taifa.
 

Chadema hawataki maradhiano ya kunywa chai

Au ya kupiga picha

Wanataka maridhiano ya ukweli
 
Katiba ni ya wananchi na sio ya CHADEMA hivyo wataandika wananchi .

Halafu sio lazima CHADEMA kushiriki maridhiano .

Mnaweza kushiriki hayo maridhiano na akina CHAUMMA , ACT .
 
Iko hivi, kwa sasa cdm ndio yenye nguvu ya wananchi. Ushahidi ni voters turn out ya umma juzi kwenye uchaguzi baada ya cdm kususia. Cdm wana kura ya turufu kwenye mchakato wa katiba, hii ni iwapo ccm inataka, ama haitaki. Na cdm wasiposhiriki automatically mchakato mzima utakosa maana tegemewa.

Na kwa kukusaidia tu, cdm wameshajua nguvu yao na wameamua kuisimamamia. Ccm wameijua nguvu halisi ya cdm baada ya uchaguzi wa juzi, japo walijaribu kujidanganya haipo. Wanachojaribu kufanya sasa ccm ni kujikaza ionekane hawaijui nguvu ya cdm, lakini ukweli ni kuwa zama za ccm zimeisha, na zitaisha kwa aibu. Mchakato wa kuandika katiba mpya unategemea uwepo wa cdm, tena ikiwa na nguvu ya maamuzi. Kama huamini subiri cdm wagomee huo mchakato kama hujaona mchakato hafifu. Cdm wasiachie hapo hapo, tena kwa huu ushindi wa kubumba wa kura 31m ndio mtafurahia show.
 
Kwa nini washiriki ulaghai? Mara ngapi wameshiriki na hakuna matokeo? Zamu hii kuna kipi kipya? Ccm wamebadilika? Tatzo la haya maridhiano ni CCM kujiona wanatoa hisani kwa wananchi na kufanya wwnye nchi kama ng'ombe tu. Wanaamua watakavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…