Elections 2010 CHADEMA wamekamilika kuongoza nchi

Godwine

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2010
Posts
1,371
Reaction score
283
Nashindwa kutambua kama ikitokea mwaka 2015 wamechukua nchi kwenye uchaguzi huo, je wana uwezo kiasi gani wa kuongoza taifa hili masikini la kizazi kilichokata tamaa na kupoteza uelekeo. maswali yangu yapo katika nyanja zifuatazo

1.Je sera zao zipoje katika kuliongoza taifa hili

2.Je muundo wa viongozi wao hupo vipi katika kuliongoza taifa hili

3.Ukomavu wa misukosuko ya kiuongozi kwenye chama chao hukoje

4.Nini mikakati yao katika kuondoa umasikini na kulinda rasilimali za nchi hii

5.Mipango yao inasemaje juu ya kushughulikia maovu ya viongozi waliopita(tawala wa CCM)
 
mkuu sera za CDM zipo wazi kabisa tena ni visible, hazipo kwenye makaratasi tu, km wewe ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za bongo naamini sera za CDM utakuwa unazijua.
 
Hivi unadhani nchi hii ina matatizo na manifesto za chama? Ni nzuri kupita kiasi, lakini utekelezaji ni kitu kingine. I am not convinced that this bunch of people have what it takes (kwa uwezo na uadilifu) kupewa madaraka. I know most people will be mad about it but thats the truth.
 

kama unayo kwenye softcopy unaweza kuiweka hadharani kwa wenye kutaka kuijua waisome online
Pitia hiyo web yao ina kila kitu unachokitaka pamoja na hiyo manifesto.

Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…