Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Ni dhahiri na wazi kabisa kuwa kwa sasa CHADEMA imefika hatua imekata tamaa kabisa ya siasa hapa Nchini,imepoteza morali,hamasa,nguvu iliyokuwa nayo miaka Kadhaa iliyopita. Kwa sasa CHADEMA imepoteza na haina kabisa ushawishi kwa watanzania.haina mvuto wala nguvu ya hamasa na kuteka mioyo ya watu.
Embu jaribu kuangalia umebaki muda mfupi sana kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika November 27 Mwaka huu,lakini ukijaribu kufuatilia maandalizi ya CHADEMA huoni kitu chochote kile kinachoendelea wala kufanyika.,hakuna hata ile hamasa kama iliyokuwepo zamani ya kuwataka watu wakajiandikishe kwa ajili ya kupiga kura,hakuna ile mikutano ya hadhara kama ambavyo walikuwa wanafanya zamani enzi za Dkt Slaa.
Mitaani huku CHADEMA imesahaulika ,kufifia na kupotea katika mioyo ya watanzania.chama kimepoteza kabisa ushawishi kwa watu.hakina ile nguvu ya Umma kiliyo kuwa kikijivunia zamani.kwa sasa hakiwezi hata kushawishi watu kushinikiza jambo fulani kufanyika au kubadilishwa na serikali.kwa sababu hakina watu wa kufanya hivyo wala kuleta presha ya kushinikiza jambo.
Na hapa mnaweza kurejea suala la kufanya maandamano lilivyoshindikana na kumuacha mbowe na mkewe na mwanaye ndio waandamane ,huku vijana wote na viongozi mbalimbali akiwepo katibu mkuu wakiingia mitini na kuendelea na shughuli zao .kama ambavyo mlishuhudia Mnyika akiendelea na ratiba zake za kanisani.
Jaribu kufikiria ni sera ipi na ajenda zipi wanazosimamia CHADEMA kwa sasa? Ni sera na ajenda zipi zinazoongozwa na CHADEMA zenye kugusa hisia za watu? Ni nini wanachozungumzia CHADEMA kwa sasa chenye kugusa maisha ya watu hadi mtu ashawishike kuwaunga mkono na kupanga kuwapa kura? Ni sera na hoja ipi ya CHADEMA kwa sasa unayoweza kusema imeleta na kuteka mijadala ya kisiasa mitaani? Ni hoja ipi ambayo imetolewa na CHADEMA wakati huu na ikaungwa mkono na watu na kuwa gumzo na kugusa mioyo ya watu na kutaka serikali iifanyie kazi?
Sasa kama chama hakina sera wala ajenda wala hoja zenye mashiko na kugusa watu ,ni vipi sasa kitapata kura? Ni vipi sasa kitashindana na CCM chama chenye mizizi mirefu mpaka huko vitongojini? Ni vipi sasa CHADEMA itashindana na CCM yenye mtandao wa uongozi kila eneo hapa Nchini? Ni vipi sasa CHADEMA inaweza tunishiana Misuri katika sanduku la kura chama ambacho kimetekeleza vizuri ilani yake ya uchaguzi?
Ni vipi CHADEMA inaweza shindana na CCM hii imara na madhubuti yenye kuungwa mkono na watumishi wote wa umma,wafanyabiashara, wakulima,vijana ,akina mama,wazee,wanawake na makundi mbalimbali? Ni vipi CHADEMA inaweza kushindana na CCM hii yenye uwezo wa kuweka mawakala hata wawili wawili kila kituo Nchi nzima? Ni vipi CHADEMA hii ambayo inashindwa hata kulipia kodi ya ofisi zake mikoani iweze kushindana na CCM hii yenye nguvu ya kiuchumi na yenye kila aina ya vitega uchumi kuanzia viwanja vya michezo,fremu za maduka n.k.huku pia ikiungwa mkono na watu mbalimbali wenye uwezo mkubwa wa kiuchumi na kifedha?
Ikumbukwe ya kuwa kwa sasa CHADEMA ni dhaifu na dhoofu kuliko wakati mwingine wowote ule katika Historia ya mfumo wa vyama vingi.Haina umoja wala mshikamano na hivyo haiwezi kupanga mikakati na mipango ya pamoja .ndio maana unaona watu kama Lissu wakitoka hadharani kulalamika juu ya kuingia kwa rushwa ndani ya CHADEMA. Sasa kama chama hakina umoja ni vipi kinaweza kushinda Uchaguzi wakati ushindi unapaswa kuanzia ndani ya chama?
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.