leo nimesikiliza radio, na nimeona comment yako kuhusu 4R. swali ni kwamba amri hii ya hili sekeseke ni ya mwenye 4R mwenyewe au watu wengine (kama ni ya watu wengine ndo wanapambana nae direct kwa kuihujumu 4R)
ndo nilipomkumbuka jiwe na kauli yake.
au mawazo kama yangu ndo yanasaidia viongozi wasipate tabu? maana watanzania ndo sisi
..swali lako limeibua mambo mengi sana kichwani kwangu.
..Kwa mtizamo wangu 4R ni maneno tu ambayo hayana utekelezaji wowote ule.
..Hakuna hujuma yoyote ile kwasababu hata Raisi mwenyewe hakuonyesha hatua za dhati kwamba amemaanisha tuwe na 4R.
..4R ilitakiwa zitanguliwe na uteuzi wa wasaidizi wanaoendana na falsafa hiyo. Kwa mfano, Raisi alipaswa ateue IGP, DCI, DPP, Msajili wa vyama, ...ambao rekodi zao zinatia imani kwamba watatekeleza 4R.
..Raisi alipoteua maofisa ambao walihusika na mambo ya hovyo ktk awamu ya Magufuli nilikata tamaa kwamba hana nia ya dhati na 4R.
..Ushahidi mwingine ni kuhusu sheria ya mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi uliopitishwa na Bunge na kusainiwa na Raisi.
..Wadau walijitahidi kutoa maoni yenye tija. Kwa bahati mbaya sehemu kubwa ya maoni hayo imetupiliwa mbali. Matokeo yake yamefanyika mabadiliko ambayo sio ya msingi na hayajakidhi kiu ya wadau wa uchaguzi na demokrasia.
..Ningeweza kuendelea, lakini kwa uchache hicho ndicho kinachoendelea kuhusu 4R. Kwa kifupi ni ulaghai tu.
NB:
..Kuhusu mtafaruku uliotokea Mbeya inawezekana kabisa sio amri ya Raisi. Lakini Raisi lazima atakuwa amepewa taarifa za kinachoendelea. Na kwasababu amri hizo hazikubadilishwa, maana yake Raisi amebariki.