CHADEMA wameshatolewa kwenye reli, Vita ya ufisadi na Katiba Mpya siyo sera zao tena

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
CCM wanajua siasa na kimsingi ndio chama pekee cha siasa nchini.

Jiulize baada ya CCM kuzitekanyara sera za Chadema ile Vita ya mafisadi iliyoasisiwa na Dr Slaa ft Tundu Lissu pale Mwembe Yanga na hii ya Katiba mpya sasa Ufipa wamebki na nini?

Mambo ya Katiba mpya sass CCM imeyabariki na kuwapeleka Kikosi kazi cha Prof. Mkandalla na Zitto Kabwe hivyo Pambalu na Mwaipaya wa Bavicha hawana kazi tena za kuzunguka nchi nzima.

Mungu ni mwema wakati wote.
 
Wewe Ni kazi bure, hasara tupu
 
Siasa ni sayansi, na CCM ni wanasayansi.

Kweli ccm ni chama cha wazee na wanawaza kizee mno, hapo walipo wenzao hayo mambo waliwaza muda mrefu, wao ndio wanaamka sasa na kuyarukia! Na kwa bahati mbaya wanadhani wakirukia hizo ajenda ndio watapata mvuto.
 
Kachukue posho yako kwa Mhasibu
 
Kwa hiyo CCM haina Sera inachukua za Chadema ili kuzifanyia kazi .
 

Nenda kamsikilize mnyeti.
 
Kwa hiyo CDM wakalale? Vita ya katiba ndio kwanza inapamba moto. Kuna mchakato na kuna maudhui vyote hivyo vyahitaji kufanyiwa kazi. Naona wapiga ramli.
 
Maana yake ni kuwa hii ni hatua NZURI muhimu, kwani ujumbe wa uhitaji wa Katiba mpya SASA umefika.

 
Unadhani hatukumbuki maneno ya ccm kuwa katiba hapana ati wanajenga nchi, pia wadhan hatujui harakati za bavicha ya akina pombal na mwaipaya juu katiba mpya mpaka sasa ccm wameufyata na kuikubali.

Watakao kuamini kwa maneno yako haya ya ghiriba ni wazee na vibabu vyako ulivyoviacha uko kijijini kwenu, sisi ukweli tunaujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…