CHADEMA wana hoja gani kwa sasa?

CHADEMA wana hoja gani kwa sasa?

Kajeba

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2020
Posts
1,057
Reaction score
2,364
Niko najaribu kuhusianisha mafanikio ya Mama na uwepo wa hoja za kimaendeleo kutoka vyama pingapinga hususani CHADEMA.

Miaka mitano iliyopita wapinzani walinyanyaswa sana, walipewa kesi za uongo, walifungwa jela pia mali zao zilitaifishwa.

Wapinzani hao hawakuruhusiwa kufanya siasa, kila walipokanyaga walikumbana na rungu la polisi, wapinzani walikuwa na hoja nyingi sana za msingi na hawakuweza kuwaambia wananchi kwa sababu ya utawala uliokuwepo.

Leo hii Mama amemaliza hayo yote ndani ya miezi mitatu tu, hao CHADEMA wanajua uchumi uko vipi, huwezi endesha nchi bila uchumi, mama anafuata vipaumbele kwanza.

Sasa hivi mbali na madai ya katiba, CHADEMA wanaagenda gani za kimaendeleo ndani ya nchi hii.
 
Back
Top Bottom