Katiba mpya kwa waTanzania itawaletea vitu vitatu muhimu
- Uhuru
- Haki
- Maendeleo ya watu
UHURU WA KWELI : Tangu mkoloni mweupe aondoke akaingia mkoloni mweusi CCM bado watanganyika na wazanzibari wanatafuta uhuru wao toka kwa wakoloni weusi. Uhuru wa kuchagua viongozi wao ngazi zote ktk utumishi wa umma na uwakilishi bungeni. Uhuru wa kuwawajibisha viongozi wazembe, wala rushwa, walioshindwa kulinda katiba n.k
HAKI : Haki katika nyanja nyingi hakuna mfano serikali ya mkoloni mweusi inasema inamiliki ardhi yote kupitia kwa rais kiasi wananchi wanaweza kubomolewa majumba, kuhamishwa bila fidia stahiki n.k n.k. Haki ya elimu bora kwa wote badala ya wengine kwenda shule za kata na kumaliza shule wakiwa raia daraja la pili kutokana na elimu isiyo ya viwango. Haki ya kupata matibabu sawa kwa wote bila kujali wewe ni kiongozi, mbunge n.k Haki ya kuwa na hospitali kubwa za kiwango cha Mlongozila, Muhimbili, Bugando ktk kila wilaya nchini.
Haki nyingine iliyopokwa ni Jeshi la Polisi halitumii PGO, ofisi ya DPP kupeleka mashtaka kwa shindikizo lisilo na haki au kufuata sheria, Mahakama na asasi zote ktk mfumo wa jinai haki (criminal justice system ) kuhakikisha watanzania wengi wasiwe wahanga wakuhangaika kupata haki.
MAENDELEO YA WATU: watanzania waweze kuanzisha biashara na shughuli zingine za kiuchumi kama ukulima, uvuvi na ufugaji bila vikwazo visivyo vya lazima kupata leseni, nyavu pia maboti ya kisasa, maeneo maalum ya ufugaji na huduma zake ili kuondokana na mapigano ya wakulima na wafugaji. Upatikanaji wa pasipoti kwa urahisi ili watanzania waweze kutoka na kuingia nchini ktk harakati za kutafuta maisha ughaibuni. Diaspora kutambulika kama kundi maalum na kupatiwa uraia pacha waweze kushiriki kuleta maendeleo kwao binafsi na kwa kushirikiana na watanzania wengine waliopo nyumbani. N.k