Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
August 4, 2020 kulikuwa na mkutano mkuu CHADEMA, TV stations karibu zote hawakushughulishwa na walau kulifanya mubashara pia zilijitokeza online media chache nadhani hazikuzidi tatu waliojitoa kurusha tukio hilo, Mwananchi aliondoka na sauti aidha kwa bahati mbaya au maksudi.
Livestream ya hotuba ya Lissu kwenye Digital Mwananchi iko censored?
Pia August 5, 2020 ITV Superbrand Afrika Mashariki kwenye mkutano mkuu wa ACT Wazalendo, alikaribishwa Tundu Lissu kwenye mkutano huo na punde alivyoanza kuongea, ITV waondoka na sauti aidha kwa maksudi au bahati mbaya lakini pamoja na yote hawajawahi kusumbuliwa wala kufungishiwa virago kwenye majambo yoyote yahusuyo CHADEMA.
ITV siyo sahihi kutoa sauti ya Hotuba ya Tundu Lissu katika Mkutano wa ACT-Wazalendo
Pia nimesahau kidogo muktadha lakini nakumbuka ITV walilipwa na CHADEMA kurusha jambo fulani mubashara, tukio lilipopata moto walianza kuondoka na sauti na baadae kutokomea moja kwa moja kusikojulikana.
Si lengo kusimama na TBC kwa matatizo yake ya uhanahabari na CHADEMA au upinzani kwa ujumla, lakini CHADEMA inaikalia sana kooni TBC kwa matatizo ambayo wengine wanayafanya lakini hawachukui hatua kama ambazo wanazichukua kwa TBC.
Vyombo habari vya binafsi vilitakiwa kuwa huru zaidi kufanya 'coverage' ya upinzani kwa sababu mmiliki wake sio serikali ambayo inaongozwa na chama cha Mapinduzi lakini pamoja na makosa yao, mnaenda kumshikia bango mtu ambaye structure yake ya ufanyaji kazi tayari imembana hata akipenda apindue meza hatoweza. Mnyonge mnyongeni...