LGE2024 CHADEMA wanatoa Tamko kuhusu hali ya Kisiasa inayoendelea nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 CHADEMA wanatoa Tamko kuhusu hali ya Kisiasa inayoendelea nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kimewaalika waandishi wa habari katika makao makuu ya Mikocheni kutoa tamko kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea hivi sasa nchini.

View: https://www.youtube.com/live/ELiZW0Fm5y4

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, amesema hawana mpango wa kujitoa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 licha ya kudai kumekuwa na changamoto nyingi zinazokandamiza Chama chao.

Ameongeza kuwa, "CHADEMA, kitaendelea kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hata kama Wagombea wao wote wataenguliwa kuelekea kwenye Uchaguzi huo"

Kuhusu Wagombea walioenguliwa kwenye Kinyang’anyoro

"Tunatoa maelekezo maeneo ambayo mpaka saa nane na nusu wagombea wetu wa uchaguzi wa serikali za mitaa wameenguliwa tunaelekeza wagombea, viongozi wa Chama na Wanachama popote walipo waondoke waende kwenye ofisi za Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, hapa natoa taarifa lakini kwenye mfumo wetu wa kichama Shinyanga wameshakwenda, Sirari kule Tarime wameshakwenda, kama Mbeya na Dar es Salaam hasa maeneo ya Segerea wameshakwenda"

"Pili, wagombea wa CHADEMA wa uchaguzi wa serikali za mitaa walioenguliwa kinyume na kanuni wakate rufaa kwa mujibu wa kanuni ya 23 ila wakati wagombea wanaendelea na mchakato wa rufaa wanachama na viongozi wetu wachukue hatua watakazoona zinafaa kutokana na maeneo yao ikiwemo kuwataka watendaji wa mitaa vijiji na vitongoji wawaeleze sababu za kuwaengua wagombea wetu"

"Chama (CHADEMA) kitakaa vikao vyake hivi karibuni baada ya zoezi hili la kuengua na kutengua na tutatoa taarifa rasmi lakini kujitoa sio sehemu ya msamiati wetu katika uchaguzi huu (uchaguzi wa serikali za mitaa 2024), kwetu kushinda mtaa mmoja ni ushindi wa asilimia 100"

"Kibamba hapa Dar es Salaam wapo wagombea wetu wa uchaguzi wa serikali za mitaa walioenguliwa sababu eti kwamba hana kazi ya kumpatia kipato halali, ni kwa sababu wameandika ni wajasiriamali sasa unajiuliza sijui walitaka watu wetu wadanganye kuwa ni wakulima ili mwisho wa siku waseme Dar es Salaam hakuna mashamba"

Aidha, ameongeza kuwa, "Kilosa kule mkoani Morogoro wagombea wetu (wa uchaguzi wa serikali za mitaa) wameenguliwa bada ya fomu zao kuchezewa, wasimamizi wamesahau kwamba mwaka huu (2024) wagombea walikuwa wanajaza fomu mbili, kwa mfano mgombea kwenye kata ya Kimamba 'B', kijiji cha Kimamba 'B', kitongoji cha Kwa Bwana Mizinga mgombea wetu anaitwa Kilato Yunge Boniface badala ya Yunge wameongeza herufi moja anaandikwa kama Myunge, badala ya Boniface ameandikwa Boneface"

"Kanda ya Serengeti hususani Bariadi vijijini bado hawajabandika (majina na fomu za wagombea waliopitishwa na mamlaka ya kusimamia uchaguzi yaani wale waliokidhi vigezo) mpaka kufikia majira ya saa saba mchana huu (leo, Ijumaa Novemba 08.2024), kuna maeneo wamebandika na kwingine bado kuna kitu kipya kimetokea wakati kanuni ikiwataka wabandike fomu za wagombea ili mgombea akiona fomu imekosea waweze kuweka pingamizi"

"Wasimamizi wamekuja na orodha ya majina ya kwamba hawa wameteuliwa, hawa wajateuliwa ili tuweze kujua huyu ni mwenyewe au la, wanafanya hivyo kuficha baadhi ya madhaifu yao, na udhaifu mmoja wako uko Meatu mkoani Simiyu ambapo kwenye wilaya hii yupo mgombea kutoka Chama cha Mapinduzi ambaye hana sifa amegombea, kwanza ni Diwai wa CCM na ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meatu amegombea katika kijiji kama Mwenyekiti wa kijiji wakati kanuni zinamkataza, yeye ameenda kuchukua fomu na amegombea akiwa Diwani"

Pia, Soma:

John Mrema aanika madudu ya TAMISEMI, waongeza sifuri na herufi kuwakosesha sifa Wagombea
Wagombea wa CHADEMA waenguliwa kwenye kinyang'anyiro kisa hawana kazi ya kuwapatia kipato halali
 
Chama kisichoweza kufikisha hata wanachama 20 kikiitisha maandamano hicho hakiwezi kutoa tamko
 
Wanaleta mambo yaleyale ya Magufuli na huu ni Uchafuzi mdogo hebu fikiria huo Uchafuzi Mkuu?!🤔
 
Back
Top Bottom