CHADEMA inamshutumu Amosi Makala ikidainalieleza Uma kuwa CHADEMA ina mpango wa kununua Virusi vya kuangamiza Wanachama wa CCM.
==========
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeagiza wanasheria wake kuwafungulia mashtaka, waliohusika kusambaza taarifa zilizodai kuwa CHADEMA, wamenunua virusi hatari na kusambaza kwa wananchi, taarifa ambayo inahatarisha usalama wa nchi na kuwatia hofu watalii kuja nchini kutalii.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Bara, Mh. John Heche, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanya vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.