figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Mapema leo tarehe 28 Februari 2025 viongozi wakuu wa Chama wakiongozwa na mwenyekiti Taifa Tundu Lissu wametembelea Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre - LHRC) na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi Wakili Fulgence Masawe.
Hii ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya viongozi kukutana na taasisi mbalimbali na watu mashuhuri kufanya nao mazungumzo na kufikisha ujumbe wa #NoReformsNoElection.
Mwenyekiti ameambata na Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. HecheJohn, Katibu Mkuu Mnyika na Naibu Katibu Mkuu Bara Amani Golugwa.