Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,207
- 17,674
Mwenyekiti wa bavicha na mgombea kiti cha uenyekiti wa Chadema kanda ya Victoria John Pambalu amemtuhumu mshindani wake bwana H Wenje kuwa alihonga wajumbe na pia alisafirisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali kuja Bukoba kupiga kura.
Tuhuma hizo zilimfanya Pambalu kususa na kuondoka akiwa na kundi lake na kuacha uchaguzi ukiendelea ambapo bwana Wenje alishinda kwa kura nyingi.
Akijibu tuhuma hizo bwana Wenje amemkejeli Pambalu kuwa alikuwa anajua atashindwa na hivyo kususa kwake hakumnyimi usingizi. Bwana Wenje amemtaka John Pambalu kukata rufaa kama kweli anaamini alifanyiwa rafu kwenye uchaguzi huo.
Source: Mwananchi