PendoLyimo
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 969
- 1,055
CHADEMA WAZIDI KUVURUGANA VIJANA WA CHASO IRINGA NAO WATOA MSIMAMO MKALI KUHUSU SUALA KATIBA MPYA.
Katika hali isiyo ya kawaida vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kutoka mkoa wa Iringa wametoa tamko kali kuhusu suala la mchakato wa katiba mpya, mchakato ambao wao kama chama ndiyo wameushikia kidedea licha ya mh Rais kuonesha nia na kwamba wampe muda kwasababu kwanza ndiyo ametoka kupokea kijiti kutoka kwa hayati Dr. John Pombe Joseph Magufuli hivyo anahitaji muda wa kutengeneza uchumi kwanza halafu suala hilo litafuata, jambo ambalo viongozi hao wa juu wa chadema wameligomea kabisa.
Vijana hao ambao wameviambia vyombo vya habari mkoani Iringa kwamba hawapingi suala la katiba mpya katika nchi yetu lakini kinachowafanya watilie mashaka vuguvugu hili ni kwamba halijawahi kuwa kipaumbele chao kuanzia katika sera zao hadi ndani ya katiba yao ya chama jambo ambalo vijana hao wa chadema wanaona kama ni suala la kisiasa lakini siyo takwa la wananchi kama chadema wenyewe wanavodai.
Katiba ya CHADEMA imepuuza vitu vingi sana ndani yake kama vile haina ukomo wa uongozi ndo maana mpaka kesho utakuta mwenyekiti wa chama hicho ni Freeman A. Mbowe pekee na hajawahi kuruhusu mtu mwingine achukua hatamu ya kuongoza chama hicho kongwe hapa nchini kilichoanzishwa tangu miaka ya 1992 huko, vilevile katiba ya CHADEMA haijawahi kuruhusu mwanachama wake yeyote kuhoji chochote kinachoamuriwa na viongozi wa ngazi za juu na kama itatokea mwanachama huyo kufanya hivyo basi ategemee kufutwa uanachama au kuitwa msaliti tuna mifano mikubwa sana ya baadhi ya viongozi kama mtakumbuka akina Zitto Zubery Kabwe, akina Kitila Mkumbo na wengine wengi lakini kwa Iringa pia kuna watu walikihama chama hicho kwasababu ya malumbano ambayo yalikuwa yanakandamiza uhuru wao wa kuongea ndani ya chama hicho
Ukiritimba, ubabe na uonevu uliokithiri ndani ya CHADEMA ni jibu tosha kabisa kwanini vijana wanaanza kutofautiana kimawazo na mwenyekiti wao jambo linalokwamisha kabisa harakati zao za kudai katiba mpya kwasababu zimekuwa ni mbio za kisiasa na wala si takwa la wananchi. Udumavu na ubovu wa katiba ya CHADEMA unawapa maswali mengi sana ambayo majibu yake ni kumfanya kiongozi fulani kuwa kama Mungu mtu na asiyeweza kubadilishwa au kupokelewa kijiti hicho cha kuongoza chama kinachojiita kina demokrasia kumbe ni udanganyifu mkubwa kazi kutafuta ajenda mfu na kuanza kuzisimamia mpaka sasa wanapoteza sifa ya kuwa chama cha watetezi na kuwa chama cha watetea matumbo yao kiufupi hawana jipya.
Siasa za hovyo zisizo kuwa na msingi, siasa ambazo haziheshimu maoni ya wanachama wake limekuwa jambo lenye kukatisha tamaa ndo maana kwa asilimia kubwa ya wanachama wake wanahoji ubora wa katiba yao kwanza kabla hawajaingia kudai katiba ya nchi. Yaani huwezi ukawa unang'ang'ana kutoa kibanzi kwenye jicho la ndugu yako wakati katika macho yako kuna boriti hapo lazima CHADEMA wajitafakari kwanza wajipange upya halafu ndipo waje kutuambia kuhusu katiba mpya.
Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia njema anaomba apewe muda na atalifanyia kazi suala hilo lakini CHADEMA wamekuwa wakaidi na kushindwa hata kuheshimu mamlaka ya Taifa hili jambo ambalo limekwaza wengi sana hasa watanzania wa kawaida wanaoipenda nchi yao lakini wenye mapenzi mema kwa Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rai yangu Chadema wanapoona haya mambo wanatakiwa kujitafakari siyo kuanza kutupiana mpira kuwa hizi ni propaganda bali waone ni changamoto wanazopaswa kuzifanyia kazi na siyo kuzipuuzia vinginevyo wataonekana kama chama cha kihuni na vijana hatutakubali kejeli na matusi kwa Rais wetu au mtu yeyote atakaye jaribu kuvuruga amani ya Taifa hili basi tutalala nae mbele. Ahsante.