Baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, kudai kuwa chama hicho kimezuiwa kufanya mkutano wake uliopangwa kufanyika jioni ya leo, Februari 27, 2025, katika hoteli ya Sea Cliff, sasa maandalizi ya Mkutano huo Mkubwa wa chama hicho yanaendelea Makao Makuu, Mikocheni.
Updates!
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA), Tundu Lissu usiku huu February 27, 2025 amezindua Mkakati Maalum wa Kigitali wa CHADEMA uliopewa jina la ‘Tone Tone’ unaolenga kuhakikisha Wafuasi wa CHADEMA na Watu wengine wanakichangia Chama hicho fedha kidogodogo ambayo ikikusanywa kwa Watu wengi itakuwa nyingi na kusaidia shughuli mbalimbali za Chama.
=========================
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Fedha ya chama hicho Godbless Lema ameeleza kuwa mkakati wa Tone Tone ni mpango wa kuchangia fedha kwa chama kwa kutumia mifumo ya kidigitali ambayo utamuwezesha mtu yeyuote kuchangia kwa kutumia mitandao ya simu na malipo ya kurudia rudia.
Lema ameeleza kuwa kupitia tone tone mtu yeyote ataweza kutoa fedha kidogo aliyonayo na pale zitapounganishwa zitajaza na kufikisha kiasi ambacho kitakiwezesha chama kuweza kuendesha mikakati yake.
Aidha amefafanua kuwa watu wataweza kujiunga na mkakati huo kupitia ku-subscribe kwenye mitandao ya kijamii kama instagram, pia kuweka malipo ya kujirudia rudia(standing order) kupitia mitandao ya simu.
Mwenyekiti wa Kamati ndogo ye fedha ya CHADEMA CHADEMA ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Godbless Lema amesema wapo tayari kutumia mfumo wa sarafu za kidijitali (cryptocurrency) ili kuweza kukusanya michango ya kwenye mkakati wa Tone Tone.
Aidha Diaspora wamefanya kazi kubwa na lengo letu hadi Mwezi wa tano tufikishe Diaspora 1000 na tuna mpango wa kufungua kama NGOs kule wawe wanakatwa moja kwa moja kila mwezi, nawasihi Watu wote Nchi nzima, ‘Tonetone’ kidogokidogo “
Baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, kudai kuwa chama hicho kimezuiwa kufanya mkutano wake uliopangwa kufanyika jioni ya leo, Februari 27, 2025, katika hoteli ya Sea Cliff, sasa maandalizi ya Mkutano huo Mkubwa wa chama hicho yanaendelea Makao Makuu, Mikocheni.
Baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, kudai kuwa chama hicho kimezuiwa kufanya mkutano wake uliopangwa kufanyika jioni ya leo, Februari 27, 2025, katika hoteli ya Sea Cliff, sasa maandalizi ya Mkutano huo Mkubwa wa chama hicho yanaendelea Makao Makuu, Mikocheni.
Haijalishi. Muhimu ni muonekano machoni mwa watu. Hayo ya nyuma ya pazia hayana tija.
Na ninajua huyo mwenye hoteli hawezi kusema wazi kuwa amewapa ukumbi bure. Mnaonekana tu ni watu wa matumizi. Huu ulikuwa ni wakati wa kujitofautisha na CCM.
Juzi ilizinduliwa uchangiaji wa TONE TONE na hivyo tunaiomba CHADEMA irudie taratibu wa uchangiaji huu mara kwa mara ili wanaopenda kuchangia wachangie.
Chama kielekeze wazi taratibu za njia rahisi kutuma mchango huu kwa njia mitandao ya simu kama vile Mpesa, Airteli, Tigo nk na njia zingine zote jinsi itakavyoona inafaa. Ili wananchi waendelee kufahamu utaratibu huu basi kila mara matangazo ya uhamasishaji yawe yanatolewa.