Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Katika pita pita zangu nikajikuta nimetembelea tovuti yahttp://www.chadema.net na mara moja macho yangu yakavutwa kama na sumaku na maneno haya yaliyo katika ukurasa wa mbele.
Nilipoyasoma mara ya kwanza niliyapita bila kuyatafakari. Niliporudia tena na nikizingatia kuwa kama ni mtu ambaye ni mgeni na ninapita kujifunza kuhusu chama nikabakiwa na hilo swali..:
What is wrong with this?
Nilipoyasoma mara ya kwanza niliyapita bila kuyatafakari. Niliporudia tena na nikizingatia kuwa kama ni mtu ambaye ni mgeni na ninapita kujifunza kuhusu chama nikabakiwa na hilo swali..:
What is wrong with this?
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama mbadala kinachokua na kinachoongozwa kwa Falsafa ya "Nguvu ya Umma" na kuamini katika itikadi ya "Mrengo wa Kati". CHADEMA kinataka Watanzania waelewe kuwa Mabadiliko ya kweli yataletwa kwa kubadilisha mfumo mzima wa utawala. Maendeleo ya kweli hayawezi kuletwa na mafisadi walewale, wa chama kilekile, chenye uoza uleule, wakiendeleza yaleyale kwa ari, nguvu na kasi mpya. Haya yamethibitishwa na Serikali ya awamu ya nne kwani sera na juhudi zao zimeambulia kutuletea usanii mpya, maahadi mapya na hakuna jipya; Kwao maisha bora ni kwa kila fisadi!