Pre GE2025 Chadema yaahidi Ushindi wa kishindo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Dar es Salaam

Pre GE2025 Chadema yaahidi Ushindi wa kishindo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Dar es Salaam

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Uongozi mpya wa Chadema DSM umeahidi Ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa

Ahadi hiyo imetolewa na viongozi wa Ilala, Kinondoni na Ubungo kwamba hakuna Mtaa utabaki CCM Baada ya Uchaguzi

Source: Mwananchi

==============

Dar es Salaam. Wenyeviti wapya wa mikoa ya kichama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Ubungo, Kinondoni na Ilala wamesema kipaumbele chao ni kuhakikisha chama hicho kinanyakua viti vingi vya Serikali za mitaa katika maeneo yao.

Wamesema hayo leo Jumamosi Aprili 6, 2024 wakizungumza na Mwananchi Digital baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi ulioanza kufanyika Aprili 2 hadi 5 katika mikoa hiyo ya chama hicho.

“Shabaha yangu ni kuhakikisha tunakwenda kushinda uchaguzi wa Serikali za mitaa Mkoa wa Kinondoni, sambamba na kufanya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka kesho,” amesema Henry Kilewo ambaye ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kinondoni.

Kilewo amesema katika kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa viongozi wa Chadema Mkoa wa Kinondoni, wataanza operesheni ya kushuka chini kwenye mitaa 106 kwa lengo la kuonana na wananchi na viongozi wa chama hicho.

“Mkakati wetu ni kufanya ziara ya kushuka chini kuonana na wananchi kuwaonyesha ili wawajue mapema wagombea wetu wa Serikali za mitaa ambao wameshatia nia ya kuwania nafasi hiyo,” amesema Kilewo.
Maelezo ya Kilewo hayakuwa mbali na mwenyekiti mpya wa Chadema Mkoa wa Ilala, Waziri Mwenyevyale amesema mkakati wao ni kuwaunganisha wanachama wa chama hicho kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa.

“Nikishirikiana na viongozi wenzangu tutafanya maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mapema ili kuhakikisha tunapambana na kushinda katika uchaguzi huu.

“Tunajiandaa mapema ili tuwe tayari kwa uchaguzi huu utakaofanyika mwisho mwaka huu, kwa umoja wetu ili tutalifanikisha,” amesema Mwenyevyale.

Mwenyekiti wa Chadema Ubungo, Amos Maziku amesema malengo yake ni kuchukua majimbo mawili ya mkoa huo, udiwani wa kata 14 na viti vya Serikali za mitaa katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu.
“Uchaguzi wa Serikali za mitaa ni muhimu kwetu kwa sababu ndio unatuwekea msingi katika chaguzi zingine, tunataka tushinde kwa asilimia 90.

“Chama kipo kila sehemu kuanzia ngazi za mitaa, tutahakikisha tunawapelekea viongozi bora waliopikwa na watakaoleta ushindani katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, naamini tutafanikiwa namuomba Mungu atusaidie,” amesema Maziku.

Katibu wa Kanda ya Pwani inayounda mikoa hiyo, Jerry Kerenge ameliambia Mwananchi kuwa Kileo na Maziku wamefanikiwa kutetea nafasi zao katika uchaguzi huo.

Hata hivyo, Kerenge amesema mikoa ya chama ya Temeke, Pwani Kusini (Mkuranga, Rufiji, Kibiti na Mafia) na Pwani Kaskazini (Chalinze, Bagamoyo, Kisarawe na Kibaha), ndio imebaki kukamilisha mchakato huo.
“Mikoa iliyobaki ikikamilisha chaguzi tutaamia ngazi ya kanda,” amesema Kerenge.

Katika uchaguzi huo, Kerenge amesema wajumbe waliwachagua makatibu wa mikoa ya Ilala, Kinondoni na Ubungo wanaosubiri kuthibitishwa kwa mujibu wa taratibu za chama hicho.

“Katika Mkoa wa Kinondoni, aliyeshinda ni Dani Mtanga, Ubungo (Pollyn Msofe) na Ilala Jerome Ulomi wanaosuburi mchakato wa kuthibitishwa,”amesema Kerenge.

Mwananchi
 
Shida ya CHADEMA haijifunzi. Ngoja CCM iwaoneshe kazi. Wamesahau mabegi ya kura yalikamatwa ila hakuna kilichofanywa.
 
Uongozi mpya wa Chadema DSM umeahidi Ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa

Ahadi hiyo imetolewa na viongozi wa Ilala, Kinondoni na Ubungo kwamba hakuna Mtaa utabaki CCM Baada ya Uchaguzi
Hongereni Temeke kwa kuwanyoosha Chadema Hata maandamano ya Chadema ya mkoa wa Dar rs salaam .Temeke waliiachac hawakuthubutu maandamano ya Chadema kuanzia Temeke

Temeke kwa Dar es salaam wanajielewa kuliko huko kwingine
 
Inawezekana tatizo ni kuwa watu wengi wamekuwa wapumbavu
 
Uongozi mpya wa Chadema DSM umeahidi Ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa

Ahadi hiyo imetolewa na viongozi wa Ilala, Kinondoni na Ubungo kwamba hakuna Mtaa utabaki CCM Baada ya Uchaguzi

Source: Mwananchi
waskize vizuri tena wamesema,
ni kushindwa kwa kishindo au kuangukia pua kwa kishindo au kushinda njaa kutwa 🐒
 
CHADEMA si waliwaita ACT CCM B kwa kuamua kushiriki chaguzi? sasa na wao wameamua kuwa CCM C ama?
Siasa za Tanzania bwana upinzani kwa upinzani wanaoneana wivu nani ni rafiki zaidi wa CCM
 
Uongozi mpya wa Chadema DSM umeahidi Ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa

Ahadi hiyo imetolewa na viongozi wa Ilala, Kinondoni na Ubungo kwamba hakuna Mtaa utabaki CCM Baada ya Uchaguzi

Source: Mwananchi
Kwa tume ipi? Hivi mbona chadema wanawaongopea wanachama wao kama Simba??
 
Back
Top Bottom