CHADEMA yaanzisha Harambee ya kuchangia familia za walioshitakiwa kwa ugaidi

Mungu akuzidishie
Nami nitachangia. Wanayopitia ni udhalimu wa hali ya juu. Kumsaidia yeye aliyepo matesoni, ni ibada iliyo njema mbele za Mungu. Tujiweke karibu na kumkaribia Mungu wetu kwa kushikamana na wenye kudhulumiwa.

Nitachangia kila mwezi mpaka watakapokuwa huru. Shetani hajawahi kumshinda Mungu. Mungu atawashindia dhidi ya mabaradhuli wenye kufurahia mateso ya wanadamu wenzao.

Tunaweza kupata taarifa kwa uhakika hatima ya Lijenje?
 
Amina , Mungu akuzidishie
Erythro, fanya hivi.
1. Kuna muda maalum

2. Kuna mrejesho baada ya muda maalum?

Hii yote inaweza kuwa ni kichocheo kwa wengine zaidi kujitokeza na kuendeleza mchango.

Hata kama haya hayawezekani kwa sababu maalum, BAVICHA watumie nafasi hii ya kuwashirikisha wananchi kwa lengo/malengo mahsusi.
 
Kesho lazima niweke 20,000 kwenye hiyo account kwa ajili ya familia za hao waliobambikiwa kesi na majizi ya kura.
Yani ka elfu 20 tu mkuu?
Ebu kuwa serious bana
 
Mimi sichangii chochote, ila nawasisitiza CHADEMA hebu wajiamini hizi issue za kujishusha na kuanza kuchangiana zimepitwa na wakati sana. Inaonesha jinsi msivyoweza kujiendesha. Mimi nashauri hivi vitu mwaachane navyo mfocus na agenda kubwa za kuwatoa hao watu. Chadema sio VICOBA.
 

Habari njema inayo kuja sasa japo kwa kuchelewa sana:

CHADEMA: Bila kuwapa Makavu hakuna Katiba Mpya

Ni muhimu kuupanua uwanja huu. Kutafuta namna endelevu ya kuwa karibu na wahanga wote wa misukosuko ya namna hii wakiwamo makomando hawa.

Wahanga mikononi mwao, hao ndiyo walio mashujaa wetu #1 wa mapambano.

Mungu ibariki Chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…