Pre GE2025 CHADEMA yaingia Ileje, yatarajiwa kuwaamsha Wananchi waliopunjwa kila kitu

Pre GE2025 CHADEMA yaingia Ileje, yatarajiwa kuwaamsha Wananchi waliopunjwa kila kitu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Chadema Kanda ya Nyasa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Njombe, Rose Mayemba, Inaingia Jimbo la Ileje kwa kimbunga cha Mikutano ya hadhara mfululizo yenye lengo la kukata mnyororo wa Utumwa

Ikumbukwe kwamba Ileje ni miongoni mwa Maeneo ya kimkakati ya ccm yaliyopangwa kudidimizwa makusudi kwa kunyimwa miundo mbinu kwa lengo la kupofusha fikra za wananchi ili waamini kwamba ccm ni dini, na kwamba wakiikataa watahukumiwa na Mungu siku ya kiama.

Sasa Chadema imeona mtego huo wa kijinga na imeamua kuuvunjilia mbali kwa kuingia mazima Ileje kwa lengo la kufungua fikra za Wananchi na kuwaambia wazi kwamba, CCM si chama cha Mungu, Ni chama cha kisiasa kilichoanzishwa na Nyerere na ambacho ndio nguzo ya Dhiki, shida, Umasikini pamoja na kila ugumu wa Maisha unaowakabili Watanzania.

Screenshot_2024-07-30-18-26-54-1.png
 
Kila la kheri makamanda huko: Ila samahani mkuu Hivi Makatibu wa Kanda zote nchi nzima huwa mnawatoa wapi au kuna kachuo mahala? Wako njema sana mkichwa na uratibu wa mambo na watulivu sana na ufahamu wa mambo?.Afisa mmoja wa Polisi CCM-aliwahi niuliza swali hili na akakiri kabisa ni moja ya viongozi ambao hata akifika kwao na jambo huwapasa wajipange sana na eti huwa wanawapa upendeleo maalumu wakuwasikiliza.
 
Swali hili sitalijibu hadharani, Katibu wa Kanda 1 ya Chadema ana uwezo kuliko mawaziri 5 wa serikali ya Tanzania
 
Back
Top Bottom