Chadema yajigamba kukimbiza wapigakura Mbeya Vijini

Chadema yajigamba kukimbiza wapigakura Mbeya Vijini

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
SIKU moja baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza matokeo yanayoonyesha asilimia 65 ya wapigakura wote kutojitokeza, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejigamba kuwa asilimia hiyo ni watu waliotaka kukipigia kura chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe aliliambia gazeti hili jana kuwa watu hao ni wapenzi na wanachama wake ambao wameamua kutojitokeza kwa sababu ya chama hicho kuenguliwa.

"Wananchi hawakwenda kupiga kura kwa sababu Tume imemwengua mgombea wetu ambaye alikuwa chaguo la wengi," alisema Kabwe na kuongeza:

Kauli ya Kabwe iliungwa mkono na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, Erasto Tumbo aliyesema kuenguliwa kwa mgombea wa chama hicho na uwezo mdogo wa ushawishi kwa wagombea waliobaki, ndivyo vilivyosababisha wapigakura wengi waususie uchaguzi huo na kwamba, Tume yaTaifa ya Uchaguzi imechangia kwa kiasi kikubwa.

"Wananchi walio wengi ambao ni wapiga kura wa Chadema walivunjika Moyo baada ya kuona kuwa mtu ambaye walikusudia kumpa kura zao ameenguliwa. Wapige kura kwa lipi wakati hawakuridhishwa na sera za vyama vengine?" alihoji Tumbo.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha WAnanchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alisema uchaguzi huo ulivurugwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema CCM ilivuruga uchaguzi huo kwa kuwatumia watendaji wa mitaa, wajumbe wa nyumba kumi na wasimamizi wa uchaguzi kuchukua shahada za kupigia kura ili wawape mbolea.

"Kufuatia hali hiyo asilimia kubwa ya shahada za kupigia kura zilichukuliwa kwa wananchi na hivyo kushindwa kushirika katika kupiga kura" alidai profesa Lipumba na kuongeza:

"Suala hilo tulilitolea taarifa tangu mwanzo kwa tume ya uchaguzi na walitangaziwa kuwa waache mchezo huo, lakini kwa kweli limeathiri sana uchaguzi na kuwanyima wananchi wengi haki ya kupiga. Huu ni ubakaji wa demokrasia," alilaani Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba aliungwa mkono na Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni ya CUF, Joram Bashange aliyesema tatizo hilo limetokana na CCM kutishia kuwanyima mbolea ya ruzuku wananchi wa Mbeya.

"Huu ni mchezo wa muda mrefu sana unaofanywa na CCM, na kama hali itaendelea kuwa ya hiyo huko tunakokwenda kutakuwa na matizo makubwa sana," alisema Bashange.

Wakati vyama hivyo vikitoa madai hayo, Chama Cha Mapinduzu (CCM) kimefurahishwa na ushindi huo kikisema ni wa kishindo.

Katibu Mkuu Yusuf Makamba aliliambia gazeti hili jana kuwa hawezi kuzungumzia kasoro za uchaguzi huo kwa sababu mgombea wake ameshinda kwa kishindo.

"Sina cha kuzungumza badala ya kufurahishwa na matokeo ya uchaguzi hivyo na kuwashukuru wananchi wa Mbeya Vijijini kwa kumchagua mgombea wangu,"alisema Makamba.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wa kata ya Utengule, wilaya ya Mbeya Vijijini walisema hawakwenda kupiga kura kwa sababu hawakumuona mtu ambaye anafaa kuwaongoza.

Wakiongea na mwandishi wa gazeti hili katika maeneo mbali mbali ya kata hiyo, walisema hawakuona sababu ya kwenda kupiga kura wakati mtu waliyekuwa wanaamini anafaa aliondolewa kwenye kinyang`anyiro hicho.

"Sikiliza mwandishi, usifanye kuwa hili wewe hulijui siyo kweli hakuna mtu ambaye hajui ni kwanini watu hawakujitokeza kupiga kura, kwani hata wananchama wenyewe wa CCM siyo wote ambao walikuwa wanamkubali mgombea wao," alisema Andrew Mwakitalu.

Alisema hivi sasa wananchi wa vijijini wameamka, kwani wanajua kuchambua mazuri na mabaya na kwamba, safari hii walitaka kumchagua mtu anayefaa na siyo chama kama ilivyokuwa huko nyuma.

Mwakitalu alisema kuwa wao walikuwa na imani na aliyekuwa Chadema kuwa angeweza kuwasaidia katika harakati za kuwaletea maendeleo kuliko waliopata nafasi ya kugombea.

Naye Maria Ngogo alipohojiwa ni kwanini hakujitokeza kupiga kura wakati kulikuwa na mgombea ambaye ni mwanamke na angeweza kumuunga mkono kwa kumpigia kura alisema kuwa anachoangalia ni mtu anayefaa kuwaletea maendeleo siyo rangi ya mtu, sura wala jinsi.

John Mwang'ombe alieleza kuwa sababu iliyomfanya ashindwe kupiga kura kwa vile hakuona mtu wa kumpigia.

Uchaguzi huo ulifanyika Januari 25, mwaka huu ambapo watu waliopiga kura hizo ni 44,855 kati ya 127780 waliojiandikisha. Kura halali zilikuwa 4394, na kura zilizokataliwa zilikuwa 914.

Mgombea wa CCM Mchungaji Luckson Mwanjali alishinda kwa kupata kura 32867 sawa na asilimia 73, CUF kura 10,578 (asilimia 23) na Chama Cha Sauti ya Umma (SAU) kiliambulia kura 496 tu ya kura zote zilizopigwa.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wamehusisha kitendo cha asilimia 65 ya wapiga kura kutojitokeza na kauli mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa Chadema na kiongozi kabila la Wamalila, lililopo katika Tarafa ya Isangati wilayani Mbeya Vijijini, Golian Mpoli (90) aliyewataka wananchi wake kutoshiriki uchaguzi baada ya mgombea wa Chadema, Shitambala kuenguliwa.

Viongozi hao akiwamo Shitambala mwenyewe aliwataka wananchi hao wasipige kura badala yake wamsubiri mwaka 2010, kwa kuwa hakuna chama kati ya vilivyobaki kwenye uchaguzi kinachoweza kuwaletea maendeleo.
Source:Mwananchi
 
Back
Top Bottom