Pre GE2025 CHADEMA yakabidhiwa Ilani ya Uchaguzi kutoka kwa AZAKI 300 nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wawakilishi wa AZAKI pamoja na Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) leo, Jumatano Oktoba 8.2024 wametembelea ofisi za makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa AZAKI hizo kutembelea vyama vya siasa kwa lengo la kukabidhi Ilani

Katika ziara hiyo THRDC kwa kushirikiana na AZAKI 300 wamewasilisha na kukabidhi vitabu vya ilani ya uchaguzi wa Asasi za Kiraia kwa mwaka 2024/2029

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili katika ofisi hizo, Mratibu Kitaifa wa THRDC Wakili Onesmo Olengurumwa amesema lengo la kutoa ilani hiyo kwa vyama vyote, ni kuhakikisha mambo muhimu kwa maisha ya Watanzania yanapewa kipaumbele kuelekea chaguzi mbili zijazo yaani uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani
1728482851777.png
"Ilani hii ni mkusanyiko na mapendekezo ya mawazo chanya ambayo kwa hakika tunaamini yamezingatia mambo muhimu, ikiwa ni pamoja na uzingatiwaji wa Haki za Binadamu, uchaguzi huru na wa haki, lakini kubwa zaidi kila Mtanzania anatamani mchakato wa mabadiliko ya Katiba mpya" - Wakili Olengurumwa

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema ameipitia ilani hiyo ya Asasi za Kiraia na kwamba amejiridhisha pasipo na shaka kuwa ipo vizuri, imekidhi matakwa muhimu ya Watanzania na haina tofauti yoyote na malengo ya ilani ya chama hicho

"Kwanza nithibitishe kuwa nimeisoma ilani hii yote kabla hamjaja kutukabidhi, ipo vizuri, imezingatia na kutoa vipaumbele kwa matakwa ya wananchi na kwa kweli haina tofauti na ilani ya CHADEMA, tutaifanyia kazi kikamilifu" - Mnyika
1728482900783.png
AZAKI hizo pamoja na THRDC wapo katika muendelezo wa kutembelea vyama vyote vya siasa ili kukabidhi nyaraka za ilani ya uchaguzi ya Asasi za Kiraia mwaka 2024/2025 ambapo kesho Oktoba 10.2024 wanatarajiwa kufika ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi (CCM), Lumumba jijjini Dar es Salaam kukabidhi nyaraka hizo.

Soma:

==> Ilani ya CCM ya 2020-2025 ina viporo vingi vimalizikekwanza kabla ya kuandaa ilani ya mwaka 2025- 2030
==> Kwanini vyama vya siasa kila siku ni katiba mpya na ununuzi wa ndege? Athari za mabadiliko ya nchi kwanini hamzipi vipaumbele?
 
Wamewasaidia CHADEMA maana wao ilani yao huwa ni mgombea wao na kile kinachomjia kichwani na kutoka mdomoni akiwa jukwaani.
 
Chadema chama kikubwa sana , watawala hulala bila viatu
 
Back
Top Bottom