Nadhani Chadena wanekuwa waungwana, na wamejua kuwa hata kama watasimamisha mtu huko ni kupoteza muda na rasilimali za nchi. Jambo ambalo ningependa kuuliza kwa wana JF, huku bara Chadema na CUF ni kipi kinakubalika zaidi? Ama nije karibu zaidi Lipumba na Slaa ni nani anayekubalika zaidi? kwa nini wasiwe waungwana kama kweli ni wanamapinduzi kukaa pamoja na kumuunga mtu mmoja? sisi wana mageuzi tunachanganyikiwa. Nimemsikia Lipumba akimlaumu Slaa kwa kugombea urais, akidai kuwa anahitajika zaidi bungeni, maana yake ni nini? Je ina maana Lipumba ana imani kuwa CCM bado itashinda hivyo Slaa anahitajika kuendelea kuwasumbua ama ana maana kuwa yeye akiwa raisi andependelea Slaa amkosoe akiwa bungeni? Mimi nadhani Profesor amejaa ubinafsi. Yeye alikimbilia kujitangaza mgombea urais kupitia CUF akitegemea kuwa Chadema hawatasimamisha mgombea na kumuunga yeye mkono. Huu ni ubinasfi.
Nadhani Profesor inabidi akubali kuwa watanzania walikwishamkataa mara tatu zote, watanzania wa leo wanataka mabadiliko sio kugombea tu. Dr Slaa ni chombo kipya, na mtu aliyejizolea umaarufu mkubwa. Lipumba na CUF ni lazima wawe waungwana na kushirikiana na Chadema na kumpeleka Slaa Ikulu. Kinyume cha hapo Lipumba awe na uhakika kuwa mwaka huu kwa mara nyingine CUF itakosa hata mbunge mmoja kama kipindi kilichopita.