Kumekucha Newala Mjini.
Mbunge wa miaka mingi Newala Mzee John Mkuchika Yuko hatarini kupoteza ubunge wake baada ya Chadema kumpeleka mgombea machachari anayedaiwa kufahamika na kupendwa na wananchi wengi wa Jimbo Hilo.
Mgombea huyo wa Chadema Issa Juma Chillindima amechukua rasmi fomu leo za Uteuzi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Akiambatana na Mwanasheria wake John Mallya mgombea huyo wa Chadema akisindikizwa na wafuasi kadhaa na wananchi amechukua fomu na Kisha kuwaambia wananchi Newala Sasa ijiandae kwa maendeleo makubwa.
Wananchi wa Jimbo Hilo wamechoshwa na ubunge wa muda mrefu wa Mzee Mkuchika na wanachama wa CCM hawakutarajia Mzee huyo kurudishwa Tena kugombea.Mara baada ya CCM kumteua Tena Mzee Mkuchika wanachama wengi wa CCM walionyesha kukata tamaa na kuahidi kumuunga mkono mgombea wa Chadema.