CHADEMA yathibitisha kutoshiriki uchaguzi mdogo Ngorongoro, hadi Tume Huru ya Uchaguzi itakapopatikana

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Taarifa kwa Umma

Katibu Mkuu John Mnyika ameiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuitaarifu rasmi kuwa Chadema hakitashiriki uchaguzi wa marudio wa ubunge kwenye Jimbo la Ngorongoro na kata saba na badala yake amesisitiza kutaka iundwe Tume Huru ya Uchaguzi itakayohakikisha chaguzi zinakuwa huru, za haki na halali kuanzia katika uchaguzi wa marudio mpaka katika uchaguzi mkuu.

Kupitia barua hiyo Katibu Mkuu ameitaka Tume ya Uchaguzi iwataarifu wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi katika jimbo tajwa na kata za Handali, Bomalang'ombe, Nyalubanda, Nalasi Mashariki, Likombe , Ipwani na Naumbu kutokutoa fomu wala kufanya uteuzi kwa yoyote atayetambulishwa kinyume cha katiba ya chama na barua hii kuwa ni mgombea kupitia Chadema.

Aidha kupitia barua hiyo Katibu Mkuu ameikumbusha kwa mara nyingine Tume ya Uchaguzi kujibu barua ya Chadema ya tarehe 25 Novemba 2020 yenye kumb. Na. C/HQ/ADM/20/TU/05/14 ambapo chama kilitaka maelezo ni nani alisaini barua na fomu za waliotangazwa kuwa wabunge viti maalum na kukipatia chama nakala ya nyaraka husika kwa ajili ya kuchukua hatua kwa kuzingatia kuwa Kamati Kuu haikuwahi kufanya uteuzi wala Katibu Mkuu hajawahi kuwasilisha orodha tajwa.
1636369615090.png
 
Hatua sahihi kabisa, hakuna haja ya cdm kushiriki hayo maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Washirika hao wasioweza ushindani wa kisiasa, bali hutumia vyombo vya dola na vikundi vya Mungiki kupora chaguzi, na kuacha wananchi na vilema vya maisha, na wakati mwingine kuwauawa.
 
Chadema kinaingia katika historia ya kuvunja rekodi ya vyama pinzani duniani kuwa na sera mbadala. Mi nimeipenda sana hii sera kwani ni sera mpya kutumika duniani. Na safari hii wakisusa huko Ngorongoro na baadaye wakisusa 2025 katika serikali za mitaa na urais na wabunge hapo wazungu na dunia watakuwa wamejua.
 
Hatua sahihi kabisa, hakuna haja ya cdm kushiriki hayo maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Washirika hao wasioweza ushindani wa kisiasa, bali hutumia vyombo vya dola na vikundi vya Mungiki kupora chaguzi, na kuacha wananchi na vilema vya maisha, na wakati mwingine kuwauawa.
Washinde peke yao
 
Wamegundua wanafanya makosa...kwahiyo waendelee kufanya kosa hilohilo?KUWA NA AKILI KIDOGO TU HATA YA KUVUKIA ZEBRA..
Mjinga wewe, ungejua kwamba kampeni huwa ni jukwaa bora kabisa la ku shout vitu vingine muhimu na kufikisha ujumbe ungekaa kimya na uboya wako.

Usifikiri tunaokosoa humu tuna nia mbaya.

bwege wewe
 
Hatua sahihi kabisa, hakuna haja ya cdm kushiriki hayo maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Washirika hao wasioweza ushindani wa kisiasa, bali hutumia vyombo vya dola na vikundi vya Mungiki kupora chaguzi, na kuacha wananchi na vilema vya maisha, na wakati mwingine kuwauawa.
Mnaogopa uchaguzi kwani dhalimu wenu bado yupo?

Si mnapumua nyie?
 
Back
Top Bottom