PostGE2025 CHADEMA yatilia shaka mwakilishi wa UN, yataka Tume Huru ya Uchunguzi ya kimataifa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416

Chama cha Denokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres, kikieleza wasiwasi wake juu ya iwapo mwakilishi waliyekutana naye, Parfait Onanga-Anyanga, alitumwa rasmi na ofisi yake kufuatilia matukio ya kabla na baada ya Oktoba 29, 2025 au la.

Onanga-Anyanga alikuja nchini wiki moja iliyopita na alizungumza na viongozi wa Serikali akiwamo Rais SSamia Suluhu Hassan, mawaziri akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohamed Thabiti Kombo na vyama vya siasa vya CCM, CHADEMA, ACT Wazalendo.

Katika kikao chao CHADEMA wakiwakilishwa na Katibu Mkuu, John Mnyika na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Dk Rugemeleza Nshala, walieleza malalamiko yao kuhusu hali ya siasa nchini, ikiwamo chama hicho kuzuiwa kufanya kazi, vurugu za Oktoba 29, 2025 na kuhusu kesi ya Mwenyekiti wao, Tundu Lissu.

Hata hivyo katika barua hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora, John Kitoka, imeeleza waswasi kuhusu hali ya kutokuwa na upendeleo katika mchakato unaoongozwa mwakilishi huyo wa UN, Parfait Onanga-Anyanga, wakitaja uhusiano wake wa awali wa kikazi na Asha-Rose Migiro, ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa CCM.

“Ingawa hatudai kuwepo kwa ushawishi wa moja kwa moja, uhusiano huo unaibua wasiwasi halali kuhusu imani ya umma katika mchakato unaoongozwa na Parfait Onanga-Anyanga.

Kwa kuzingatia hilo, CHADEMA wameomba UN iwezeshe kuundwa kwa Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi wa Ukweli (Fact-Finding Mission), itakayoundwa na wanasheria na wataalamu mashuhuri kimataifa, ikiwa na jukumu la kubaini ukweli kuhusu matukio ya vurugu yaliyotokea Oktoba hadi Novemba 2025, pamoja na mwenendo mpana wa upotevu wa watu kwa nguvu (enforced disappearances) tangu mwaka 2015.

“Tunaamini kuwa mchakato unaojengwa juu ya ukweli, uwajibikaji, maridhiano na mageuzi ya kidemokrasia—kama ilivyowahi kushuhudiwa katika nchi kama Kenya na South Africa—unaweza kuwa njia bora kwa Tanzania kuelekea haki kwa waathirika na utulivu wa kudumu wa taifa,” imesema barua hiyo.

MY TAKE:

Nani yupo nyuma ya hii michezo michafu?

Je, hii michezo itamuokoa Samia Suluhu dhidi ya damu za Mashujaa waliokufa 29 Oktoba 2025?

Mheshimiwa António Guterres, 29 Oktoba 2025, Watawala waliua Watawaliwa ili kulinda Ulaji. Yaani Serikali iiliua wate wake ili Samia asipingwe.

CHADEMA walijipinda kutema nyongo kumbe wanampa maoni ayapeleke kwa tume ya feki ya Samia Suluhu Hassan inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mohamed Othman Chande😭😭😭
 
Ilikuwaje wakaenda kuonana naye kabla ya kujiridhisha kama ametumwa na UN na walionana naye kwenye ofisi zipi? Nyumbu ni shida sana!!

Chadema unyumbu unawapotezea wanachama wengi sana wanaojitambua.
 
Body language yake haikuonyesha kuwa ni mtu wa UN.
Kaokotwa West Africa huko!!
 
Kwamba nyinyi hamkushtuka , Yaani ccm wakubali kirahisi rahisi tu mtu kutoka UN aje bila ya kuvutana vutana na UN wakati wanajijua kabisa wao ni washtumiwa wakuu !?
Hata alipokutaka na CHADEMA... nasikia walipewa a very short notice kuwa waende au wapoteze nafasi ya kuonana naye. Nadhani lengo lilikuwa ni kuwashtukiza wasiweze kuwakilishwa na timu yenye wabobezi wa kujenga hoja na pia wasiwe na muda wa kupangilia hoja zao na ushahidi. Huyu Onyanga kwanza ni mwafrika na kama tunavyojua sisi ni kama tuna laana kwenye kutenda haki.
 
Nyumbu shida sana!
 
Ilikuwaje wakaenda kuonana naye kabla ya kujiridhisha kama ametumwa na UN na walionana naye kwenye ofisi zipi? Nyumbu ni shida sana!!

Chadema unyumbu unawapotezea wanachama wengi sana wanaojitambua.
Nyie nguruwe wa ccm tulieni maigizo yenu watanzania walishayashtukia and from now onwards mtaishi Kwa sonona sana
 
Mkuu wanaoishi kwa sonona kwa sasa ni Chadema.

Walifikiri UN itachukua hatua kwa kupitia taarifa zao za uongo na uzushi, eti watz Elfu 10+ wamekufa tarehe 29 Oct 2025, hata mjinga hawezi kukubali.

Vita inayoendelea huko Iran pamoja na kupigwa makombora kila siku sasa hivi ni siku ya 12 lakini waliokufa hawafiki hata Elfu mbili!! Akili za Kinyumbu ni shida sana!!!
 
Chama cha Denokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres, kikieleza wasiwasi wake juu ya iwapo mwakilishi waliyekutana naye, Parfait Onanga-Anyanga, alitumwa rasmi na ofisi yake kufuatilia matukio ya kabla na baada ya Oktoba 29, 2025 au la.

Onanga-Anyanga alikuja nchini wiki moja iliyopita na alizungumza na viongozi wa Serikali akiwamo Rais SSamia Suluhu Hassan, mawaziri akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohamed Thabiti Kombo na vyama vya siasa vya CCM, CHADEMA, ACT Wazalendo.

Katika kikao chao CHADEMA wakiwakilishwa na Katibu Mkuu, John Mnyika na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Dk Rugemeleza Nshala, walieleza malalamiko yao kuhusu hali ya siasa nchini, ikiwamo chama hicho kuzuiwa kufanya kazi, vurugu za Oktoba 29, 2025 na kuhusu kesi ya Mwenyekiti wao, Tundu Lissu.

Hata hivyo katika barua hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora, John Kitoka, imeeleza waswasi kuhusu hali ya kutokuwa na upendeleo katika mchakato unaoongozwa mwakilishi huyo wa UN, Parfait Onanga-Anyanga, wakitaja uhusiano wake wa awali wa kikazi na Asha-Rose Migiro, ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa CCM.

“Ingawa hatudai kuwepo kwa ushawishi wa moja kwa moja, uhusiano huo unaibua wasiwasi halali kuhusu imani ya umma katika mchakato unaoongozwa na Parfait Onanga-Anyanga.

Kwa kuzingatia hilo, CHADEMA wameomba UN iwezeshe kuundwa kwa Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi wa Ukweli (Fact-Finding Mission), itakayoundwa na wanasheria na wataalamu mashuhuri kimataifa, ikiwa na jukumu la kubaini ukweli kuhusu matukio ya vurugu yaliyotokea Oktoba hadi Novemba 2025, pamoja na mwenendo mpana wa upotevu wa watu kwa nguvu (enforced disappearances) tangu mwaka 2015.

“Tunaamini kuwa mchakato unaojengwa juu ya ukweli, uwajibikaji, maridhiano na mageuzi ya kidemokrasia—kama ilivyowahi kushuhudiwa katika nchi kama Kenya na South Africa—unaweza kuwa njia bora kwa Tanzania kuelekea haki kwa waathirika na utulivu wa kudumu wa taifa,” imesema barua hiyo.

Soma: Barua ya CHADEMA
 
Aya sasa mliua watu wangapi?
 
Swali hapo kwenu watu walikufa au hawakufa?
Na walikuwa wangapi waliokufa. Hoja inapingwa kwa hoja. Weka data jukwaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…