Chadema yatishia kujitoa kwenye mchakato wa Katiba

Chadema yatishia kujitoa kwenye mchakato wa Katiba

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHadema), kimesema hakitashiriki katika mchakato wa Katiba Mpya endapo serikali haitapeleka bungeni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ili kufuta vifungu mbalimbali kikiwamo kinachowaruhusu wajumbe wa Bunge Maalum kutoka Zanzibar kushiriki katika mijadala ya mambo yasiyo ya muungano.
Chama hicho kinataka marekebisho hayo kupelekwa bungeni kabla ya mwisho wa Aprili na isipofanya hivyo kitajitoa katika ushiriki wake katika mchakato huo.
Hayo yalisemwa jana na Msemaji wa kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, alipokuwa akitoa maoni ya kambi hiyo kuhusiana na hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2013/2014.
Pia Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai, alisema chama chake kitajitoa katika ushiriki ikiwa serikali haitafuta uteuzi wa wajumbe wa mabaraza ya Katibauliofanywa na Kamati za Maendeleo za kata.
Alisema wajumbe hao wafutwe na badala yake wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na WDC.
Pia alisema wanataka kufutwa kwa vifungu vyote vinavyohusu mamlaka ya Rais kuitisha tena Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kuwa limeshapitisha Rasimu ya Katiba Mpya kwa lengo la kufanya marekebisho katika Rasimu kabla haijapelekwa kwenye kura ya maoni.
Aidha, alisema wanataka kufutwa kwa vifungu vyotevinavyohusu mamlaka ya kikatiba na ya kisheria yatakayoiwezesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuendesha na kusimamia kura ya maoni.
Alisema Tume hiyo imeonekana kutoa taarifa kwa Rais Jakaya Kikwete na kutangaza wazi wazi kwamba haiwajibiki kwa Bunge kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.
“Zaidi ya kumtuma Naibu Katibu wa Tume, viongozi wa Tume kama vile Mwenyekiti, Makamu Mwenyekitina wajumbe wa Tume wamekataa kuhudhuria vikaovya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ili kuieleza Kamati juu ya utekelezaji wa majukumu yakekwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi,” alisema Mbowe.
Kwa upande wa wanafunzi waliofeli mitihani ya kidato cha nne mwaka jana, Mbowe alisema kambi hiyo inaitaka Serikali kueleza bungeni inampango gani wa kupunguza idadi hii ya watoto wanaobaki mitaani bila shughuli rasmi ya kufanya.
CHANZO: NIPASHE
 
Nilisha shauri huko mwanzoni kuwa CHADEMA ilipaswa kuanza mchakato wake wa Katiba Mpya ndani ya siku 100 baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 hata kama haikuchukua dola.Mchakato huu ungeenda sambamba na mchakato wa sasa.Hii ingesaidia kuwa na Katiba Mbadala ya kufanya 'comparison'. Mchakato huu wa sasa ni 'kiini macho'.Hakuna atengenezaye Katiba yakumwondoa madarakani..
 
kwa kweli cdm wana reason logically,iv tume itasemaje wagombea wa mabaraza ya katiba wachujiwe WDCs na ikizingatia wajumbe wake ni wenyeviti wa mitaa/vijiji na madiwani wakiwa wenyeviti huku watendaji ni ma ex-officials.data zinasema kwamba uchaguzi wa mwaka 2009 wa serikali za mitaa ccm ilishinda kwa asilimia 90 na pia mwaka 2010 ccm tena walishinda kwa asilimia 80. sasa WDCs zote zimetawaliwa na ccm ivyo bhasi wengi watakaochaguliwa ni ccm.kwa hyo kiukweli katba itakayotokea ni ya watu wa ccm.
 
sio watakaochaguliwa wamechaguliwa tayari. Hata wataalum na VEOs ambao ni wajumbe wa WDC kikanuni walizuiliwa kupiga kura za kuwachagua wajumbe wa mabaraza ya Katiba. Msisahau viongozi wa vijiji walipewa maelekezo kuwa hawatakiwi kuwawachagua wasio na chama pia hata wale ambao sio wanaCCM. Yaaaani kuna majembe yameachwa nje kwa sababu za kijinga eti sio wanaCCM kwa hiyo sio Watz hawastahili kuingia ktk mabaraza ya Katiba, very sad. HII INADHIHIRISHA KUWA TANZANIA NI YA KUNDI FULANI
 
ivi mpaka watu wanaonga kuna posho watakayolipwa ya kuwa wajumbe wa mabaraza???
 
NI mapendekezo muhimu sana lakini yalikuwa yatolewe mapema wakati wa kupitisha sharia yenyewe! hata utaratibu wa mabaraza ya katiba ya wilaya si ulikuwa kwenye mswada!? je haya yaliseswa!? kama yalisemwa tuna haki ya kuyadai yafanyiwe kazi, lakin kama hayakusemwa leo tunayasema haya basi we ar too late.

MM aliwahi kusema kuwa asisikike mtu yeyote analalamika kuhusu machakato wa katiba, kwa kuwa tuliukubali wenyewe na ubovu wake!
 
Hivi kwa kujuzwa tuu, ili katiba ipite ni lazima ipate kura ngapi kwa asilimia both in constitution assembly and referendum!
 
Back
Top Bottom